• HABARI MPYA

  Jumapili, Novemba 22, 2015

  NIYONZIMA: TUMEFUATA KOMBE, HATUKUJA KUUZA SURA ADDIS ABABA

  NAHODHA wa Rwanda, Haruna Hakizimana Fadhil Niyonzima amesema kwamba hawajakwenda Ethiopia kuuza sura, bali kubeba Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, Challenge 2015.
  Haruna (kushoto) ambaye timu yake ilianza na ushindi wa 1-0 jana dhidi ya wenyeji Ethiopia, amesema kwamba wamejiandaa kikamilifu na timu yao iko vizuri mno kiasi cha kutosha kubeba taji.
  “Kwa kiasi kikubwa tunataka kutumia mashindano haya kama sehemu ya maandalizi ya michuano ya CHAN, ambayo sisi tutakuwa wenyeji mapema mwakani,”.
  “Na ndiyo maana asilimia kubwa ya wachezaji hapa ni wale ambao wanacheza ligi ya nyumbani tu, yaani ambao watacheza CHAN,”amesema kiungo huyo wa Yanga SC.
  Aidha, Haruna amesema kwamba baada ya kutolewa kwenye mbio za Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi, wanataka kutumia mashindano hayo kama sehemu ya kujifariji na pia kuwafariji wananchi wa Rwanda.
  “Tumetolewa katika kufuzu Kombe la Dunia, imetuumiza, sasa hapa pia ni sehemu nyingine ya kupoza machungu yetu na ya wananchi pia,”amesema Niyomzima.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NIYONZIMA: TUMEFUATA KOMBE, HATUKUJA KUUZA SURA ADDIS ABABA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top