• HABARI MPYA

  Jumatano, Novemba 18, 2015

  RWANDA, KENYA NAZO ZATUPWA NJE MBIO ZA URUSI 2018

  KENYA nayo imeungana na majirani Tanzania kuaga mbio za Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi, baada ya kufungwa mabao 2-0 na Cape Verde leo.
  Matokeo hayo, yanaifanya Kenya itolewe kwa jumla ya mabao 2-1, baada ya awali kushinda 1-0 nyumbani.
  Mechi nyingine za leo, Rwanda imefungwa mabao 3-1 nyumbani na Libya, hivyo kutolewa kwa jumla ya 4-1, baada ya awali kufungwa 1-0 ugenini.
  Kongo imeifunga 2-1 Ethiopia, hivyo kufuzu kwa ushindi wa jumla wa 6-4, baada ya awali kushinda 4-3, wakati Mali imeshinda 2-0 dhidi ya Botswana, hivyo kufuzu kwa ushindi wa jumla wa 3-2 baada ya awali kufungwa 2-1.
  Kiungo Haruna Niyonzima wa Rwanda (kushoto) ameshindwa kuisaidia timu yake mbele ya Libya

  Senegal imeifunga 3-0 Madagascar, hivyo kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 5-2 baada ya sare ya 2-2 awali, Burkina Faso imeshinda 2-0 dhidi ya Benin hivyo kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-2, baada ya awali kufungwa 2-1.
  Ivory Coast imeifunga 3-1 Liberia, hivyo kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 4-1 baada ya awali kushinda 1-0.
  Afrika Kusini imeifunga 1-0 Angola hivyo kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 4-1, baada ya awali kushinda 3-1, Tunisia imeifunga 2-1 Mauritania hivyo kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 4-2 baada ya awali pia kushinda 2-1.  
  Misri imeifunga 4-0 Chad, hivyo kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 4-1 baada ya awali kufungwa 1-0, Ghana imeshinda 2-0 dhidi ya Comoro, hivyo kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 2-0 baada ya sare ya 0-0 awali, wakati Nigeria imeshinda 2-0 dhidi ya Swaziland na kusonga mbele 2-0 baada ya sare ya 0-0 awali na Cameroon imelazimishwa sare ya 0-0 na Niger, hivyo kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-0 baada ya ushindi wa 3-0 awali.
  Timu hizo sasa zitagawanywa katika makundi matano na kumenyana katika mtindo wa ligi, ambapo kinara wa kila kundi atafuzu Kombe la Dunia 2018.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: RWANDA, KENYA NAZO ZATUPWA NJE MBIO ZA URUSI 2018 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top