• HABARI MPYA

  Jumatatu, Novemba 16, 2015

  MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA 'AWAFUTA MACHOZI' WACHEZAJI TAIFA STARS

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na kumpongeza mchezaji wa Timu ya Taifa Stars, Thomas Ulimwengu, baada ya mchezo Jumamosi

  MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amewataka wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kutovunjika moyo baada ya sare ya 2-2 nyumbani na Algeria mchezo wa kwanza Raundi ya Pili kufuzu Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi.
  Akizungumza na wachezaji hao baada ya mchezo huo, Mhe. Samia, aliwataka wachezaji na viongozi wa Stars kutovunjika moyo kutokana na matokeo ya mchezo huo, na kuwataka kuongeza juhudi na kujituma zaidi katika mchezo wa marudiano ili ukweza kupata matokeo mazuri zaidi.
  "Japo hamkushinda, lakini tumewaona jinsi mlivyojituma, msivunjike moyo na matokeo ya mchezo, kwani tumeowana mlivyocheza kwa kujituma, hivyo naamini hata ugenini mtaweza kupata matokeo mazuri zaidi mkiwa na moyo huo huo wa utaifa, juhudi na kujituma,".
  "Mtangulizeni Mungu kwa kila jambo na kwa uwezo wake naamini mtaenda kufanya vizuri katika mchezo wa marudiano, na nawatakieni safari njema leo (jana) usiku kuelekea mchezo huo wa marudiano, sisi wazee wenu na Watanzania wote tupo nyuma yenu tunawaombe muweze kuwatoa Waarabu hawa wenye fitina kali katika mchezo wa Soka,. alisema Mhe. Samia. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimfariji Mbwana Samatta, baada ya mchezo 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza jambo na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) Jamal Malinzi
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA 'AWAFUTA MACHOZI' WACHEZAJI TAIFA STARS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top