• HABARI MPYA

  Jumapili, Novemba 22, 2015

  MBEYA CITY WAMTAKA 'STRAIKA' ALIYESAJLIWA KWA MAMILIONI YANGA SC

  KLABU tano zinazoshiriki Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara zimetuma maombi kwa mabingwa watetezi wa ligi hiyo zikimuhitaji mshambuliaji, Simon Matheo katika kipindi hiki cha dirisha dogo imeelezwa jana jijini Dar es Salaam.
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE leo, Katibu Mkuu wa Yanga, Dk. Jonas Tiboroha, amezitaja klabu hizo kuwa ni Mbeya City, Stand United, Toto Africans, Aficans Sports na Majimaji.
  Tiboroha alisema sema jana kuwa Yanga inayafanyia kazi maombi hayo kwa kuzingatia maslahi ya mshambuliaji huyo waliyemsajili kwa mamilioni lukuki kutoka KMKM ya Zanzibar.
  Matheo Anthony Simon amecheza mechi moja tu Yanga SC akitokea benchi dhidi ya Azam FC kumalizia dakika tano za mwisho

  "Matheo tulimsajili baada ya kung'ara katika mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) mwaka huu, hata hivyo bado hajapata nafasi ya kuichezea Yanga, tutaangalia tumpeleke wapi kwa kushauriana na mwalimu," Tiboroha alisema.
  Katibu huyo aliongeza kuwa pia wamepokea maombi kutoka Majimaji wakimtaka kwa mkopo beki, Pato Ngonyani.
  Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilitangaza kufungua dirisha dogo la usajili ambalo litafungwa rasmi ifikapo Desemba 15 mwaka huu.
  Matheo Anthony Simon amecheza mechi mmili tu Yanga SC akitokea benchi dhidi ya Azam FC na Mtibwa Sugar Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MBEYA CITY WAMTAKA 'STRAIKA' ALIYESAJLIWA KWA MAMILIONI YANGA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top