• HABARI MPYA

  Jumamosi, Novemba 21, 2015

  CHALLENGE YAANZA LEO, BARA YAFUNGUA DIMBA NA SOMALIA KESHO

  MAKUNDI:
  Kundi A; Ethiopia, Rwanda, Tanzania Bara na Somalia.
  Kundi B; Kenya, Uganda, Burundi na Zanzibar. 
  Kundi C; Sudan, Sudan Kusini, Malawi na Djibouti.
  MECHI ZA UFUNGUZI
  Novemba 21, 2015
  Burundi Vs Zanzibar Saa 8:00 mchana
  Ethiopia Vs Rwanda Saa 11:00 jioni
  Novemba 22, 2015
  Somalia Vs Tanzania Saa 8:00 mchana
  Kenya Vs Uganda Saa 11:00 jioni
  Novemba 23, 2015
  Sudan v Djbouti Saa 8:00 mchana
  Sudan v Malawi Saa 11:00 jioni

  Beki wa Somalia, Aden Hussein Ibrahim akimdhibiti Haroun Chanongo wa Tanzania Bara Uwanja wa Nyayo, Nairobi, Kenya katika Challenge iliyopita mwaka juzi. Kipute cha michuano hiyo kinaanza tena leo Addis Ababa, Ethiopia

  MICHUANO ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge inatarajiwa kuanza kutimua vumbi leo nchini Ethiopia wenyeji wakifungua dimba na Rwanda mjini Addis Ababa.
  Mchezo huo wa Kundi A utatanguliwa na mechi nyingine ya Kundi B, kati ya Burundi na Zanzibar.
  Tanzania Bara watatupa kete yao ya kwanza kesho, watakapomenyana na Somalia katika mchezo wa Kundi A, wakati mabingwa watetezi, Kenya watasuguana na mabingwa wa kihistoria, Uganda baadaye. 
  Mechi za mzunguko wa kwanza wa makundi zitakamilishwa keshokutwa, Sudan Kusini wakimenyana na Djbouti kabla ya Sudan na Malawi kufuatia baadaye.
  Baada ya mechi za makundi kufikia tamati, Robo Fainali zitafuatia Novemba 30 zikihusisha timu mbili za juu kutoka kila kundi na washindi watatu bora wawili kwa makundi yote. 
  Nusu Fainali zitafanyika Desemba 2 na 3, wakati mechi za kusaka Mshindi wa tatu na Fainali zitafanyika Desemba 5, mwaka huu na huo utakuwa mwisho wa mashindano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CHALLENGE YAANZA LEO, BARA YAFUNGUA DIMBA NA SOMALIA KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top