• HABARI MPYA

  Jumamosi, Novemba 21, 2015

  BARCELONA YAIPA KIPIGO CHA 'MWANA UKOME' REAL MADRID, YAICHAPA 4-0 BERNABEU

  BARCELONA imeipa kipigo cha bila huruma Real Madrid, baada ya kuichapa mabao 4-0 katika mchezo wa La Liga usiku huu Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid, Hispania.
  Mshambuliaji wa zamanai wa Liverpool, Luis Suarez amefunga mabao mawili mazuri dakika ya 11 na 74, wakati mengine yamefungwa na Neymar da Silva Santos Junior dakika ya 39 na Andres Iniesta dakika ya 53.
  Barca sasa inafikisha pointi 30, baada ya kucheza mechi 12, ikiendelea kuongoza La Liga, kwa kuwazidi wapinzani, Real Madrid kwa pointi sita.
  Nyota wa Barcelona, Luis Suarez akishangilia baada ya kuifungia mabao mawili timu yake katika ushindi wa 4-0 usiku huu Uwanja wa Bernabeu  PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Real Madrid, ilimaliza pungufu mechi hiyo baada ya Isco aliyeingia dakika ya 55 kuchukua nafasi ya James Rodríguez kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 84, baada ya kumchezea rafu mbaya, Neymar.
  Nyota wa Barcelona, Lionel Messi aliyekuwa majeruhi kwa muda mrefu, aliingia dakika ya 57 kuchukua nafasi ya Ivan Rakitic na akakaribia kufunga.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BARCELONA YAIPA KIPIGO CHA 'MWANA UKOME' REAL MADRID, YAICHAPA 4-0 BERNABEU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top