• HABARI MPYA

  Ijumaa, Novemba 27, 2015

  LIVERPOOL YAENDELEA KUNG’ARA ULAYA, SPURS NAYO YATOA ADHABU UGENINI

  MATOKEO MECHI ZA UEFA EUROPA LEAGUE JANA
  Novemba 26, 2015  
  PAOK Salonika 0-0 FK Qabala
  Club Brugge 0-1 Napoli
  Sporting Braga 2-1 Slovan Liberec
  Molde 0-2 Fenerbahce
  Marseille 2-1 FC Groningen
  Liverpool 2-1 Bordeaux
  Villarreal 1-0 SK Rapid Wien
  Celtic 1-2 Ajax
  Legia Warsaw 1-0 FC Midtjylland
  FK Qarabag 0-1 Tottenham Hotspur
  FC Augsburg 2-3 Athletic Club
  Sparta Prague 1-0 Asteras Tripolis
  FC Basel 2-2 Fiorentina
  FC Schalke 04 1-0 APOEL Nicosia
  Monaco 0-2 RSC Anderlecht
  AZ 1-2 Partizan Belgrade
  Lazio 3-1 Dnipro Dnipropetrovsk
  Lokomotiv Moscow 2-4 Sporting Lisbon
  Rosenborg 1-1 St Etienne
  Belenenses 0-0 Lech Poznan
  Besiktas 2-0 Skenderbeu Korce
  FK Krasnodar 1-0 Borussia Dortmund
  Rubin Kazan 2-0 FC Sion
  Dinamo Minsk 1-0 Viktoria Plzen

  Wachezaji wa Liverpool wakimpongeza Benteke baada ya kufunga jana PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  BAO pekee la Harry Kane dakika ya 78 limeipa Tottenham Hotspur ushindi wa 1-0 dhidi ya FK Qarabag ugenini katika mchezo wa Europa League Uwanja wa Tofik Bakhramov jana.
  Kwa ushindi huo, Spurs inapanda kileleni mwa Kundi J baada ya kufikisha pointi 10 kutokana na mechi tano ilizochea. Mchezo mwingine wa kundi hilo, RSC Anderlecht imeshinda ugenini pia 2-0 dhidi ya Uwanja wa Louis II, mabao ya Guillaume Gillet dakika ya 46 na Frank Acheampong dakika ya 78.
  Liverpool imepanda kileleni mwa Kundi B baada ya kushinda mabao 2-1 dhidi ya Bordeaux jana Uwanja wa Anfiled na kufikisha pointi tisa za mechi tano. 

  Harry Kane akikimbia kushangilia baada ya kuifungia Tottenham katika Europa League jana PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Mabao ya Liverpool yamefungwa na James Milner kwa penalti dakika ya 38 na Christian Benteke dakika ya 46, wakati la wageni limefungwa na Henri Saivet dakika ya 33.
  Mchezo mwingine wa kundi hilo, Rubin Kazan imeshinda 2-0 dhidi ya FC Sion mabao ya Blagoy Georgiev dakika ya 72 na Marko Devic dakika ya 90 Uwanja wa Kazan Arena.
  Matokeo hayo, yanazifanya zote, Liverpool na Spurs zijihakikishie kutinga hatua ya mtoano ya michuano hiyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YAENDELEA KUNG’ARA ULAYA, SPURS NAYO YATOA ADHABU UGENINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top