• HABARI MPYA

  Ijumaa, Novemba 27, 2015

  SIMBA SC WAINGIA KAMBINI ZENJI JUMAPILI KUIKUSANYIA MAKALI ZAIDI AZAM FC

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  SIMBA SC inatarajiwa kuingia kambini visiwani Zanzibar Jumapili kujiandaa na mchezo wao ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Azam FC.
  Kocha Muingereza Dylan Kerr ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE kwamba timu itakuwa huko hadi Desemba 12 itakaporejea kwa ajili ya mchezo na Azam FC.
  Katika kipindi hicho, Kerr amesema atawapa pia nafasi wachezaji walioletwa kwa majaribio ya kujiunga na timu hiyo, akiwemo kinda Hijja Mohammed.
  Amesema pamoja na mazoezi ya asuhuhi na jioni, lakini pia Simba SC itacheza mechi kadhaa za kirafiki ili kujipima kaba ya mchezo huo mgumu wa Ligi Kuu.
  Wachezaji wa Simba SC watahamishia kambi yao ya mazoezi visiwani Zanzibar Jumapili

  Kwa sasa, Simba SC inashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ikiwa na pointi 21 baada ya kucheza mechi tisa, ikizidiwa pointi moja na Mtibwa Sugar iliyo nafasi ya tatu.
  Azam FC ndiyo wanaoongoza Ligi Kuu kwa pointi zao 25, mbili zaidi ya mabingwa watetezi, Yanga SC baada ya timu kushuka dimbani mara tisa. 
  Ligi Kuu imesimama kwa sasa kupisha michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge inayoendelea nchini Ethiopia hadi Desemba 5, mwaka huu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA SC WAINGIA KAMBINI ZENJI JUMAPILI KUIKUSANYIA MAKALI ZAIDI AZAM FC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top