• HABARI MPYA

  Jumanne, Novemba 17, 2015

  MESSI AIPONEA EL CLASSICO, AANZA KUJIFUA JANA TAYARI KUWAVAA REAL JUMAMOSI

  MSHAMBULIAJI wa Barcelona, Lionel Messi jana alirejea mazoezini ikiwa ni siku tano kabla ya mchezo dhidi ya mahasimu, Real Madrid wa Ligi Kuu ya Hispania, La Liga.
  Messi anajiandaa kucheza El Clasico ya kwanza msimu huu baada ya kuwa nje ya Uwanja tangu aumie goti katika mechi dhidi ya Las Palmas Septemba, mwaka huu.
  Barca imeendelea kufanya vizuri licha ya kumkosa nahodha huyo wa Argentina, ikibebwa na washambuliaji wengine wawili nyota, Luis Suarez wa Uruguay na Neymar wa Brazil.


  Lionel Messi (katikati) amerejea mazoezini Barcelona kwa mara ya kwanza tangu alipoumia goti mwezi Septemba PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MESSI AIPONEA EL CLASSICO, AANZA KUJIFUA JANA TAYARI KUWAVAA REAL JUMAMOSI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top