• HABARI MPYA

  Jumapili, Novemba 22, 2015

  MAGRAM ENZI ZAKE ALIKUWA KOCHA BABU KUBWA, KIPENZI CHA VIJANA

  Aliyekuwa kocha wa Simba SC, Mansour Magram 'Zagallo' akiwafundisha wachezaji wa timu hiyo mwaka 1982 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Magram enzi zake pia alifundisha timu za taifa kuanzia za vijana hadi ya wakubwa, Taifa Stars na alikuwa muumini wa vijana zaidi na klabu zake zote alizofundisha mbali na Simba SC, nyingine Cosmopolitan alikoibukia kwanza kama mchezaji, Sigara na Coastal Union kote aliibua vipaji vya vijana. Magram alifariki mwanzoni mwa milenia hii mjini Dodoma akiwa ana umri wa zaidi ya miaka 80. Mungu ampumzishe kwa amani daima. Amin. 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAGRAM ENZI ZAKE ALIKUWA KOCHA BABU KUBWA, KIPENZI CHA VIJANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top