• HABARI MPYA

  Jumamosi, Novemba 21, 2015

  RWANDA YAWAKALISHA WENYEJI ETHIOPIA, YAWAPIGA 1-0

  BAO pekee la winga wa kulia, Jacques Tuyisenge (pichani kulia) limeipa Rwanda ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji Ethiopia katika mchezo wa ufunguzi wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge jioni ya leo Uwanja wa Taifa wa Addis Ababa, Ethiopia.
  Tuyisenge alifunga bao hilo kwa shuti la mpira wa adhabu nje ya eneo la penalti, baada ya yeye mwenyewe kuchezewa rafu na Nejib Sani dakika ya 55.
  Katika mchezo uliotangulia, Burundi iliifunga Zanzibar 1-0, bao pekee la Didier kavumbangu. Michuano hiyo inaendelea kesho kwa mchezo kati ya Tanzania Bara na Somalia na Kenya dhidi ya Uganda.
  Rwanda itashuka tena dimbani Novemba 24 kumenyana na Tanzania Bara, mchezo ambao utafuatiwa na mechi kati ya Ethiopia na Somalia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: RWANDA YAWAKALISHA WENYEJI ETHIOPIA, YAWAPIGA 1-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top