• HABARI MPYA

  Jumatatu, Novemba 30, 2015

  BOCCO: HAWA WAHABESHI AMA ZAO, AMA ZETU LEO

  RATIBA ROBO FAINALI KOMBE LA CHALLENGE 2015
  Novemba 30, 2015 
  Uganda Vs Malawi (Saa 8:00 mchana)
  Tanzania Bara Vs Ethiopia (Saa 10:00 jioni)
  Desemba 1, 2015
  Sudan Kusini Vs Sudan (Saa 8:00 mchana)
  Rwanda Vs Kenya (Saa 10:00 jioni)
  John Bocco (kulia) amesema watapambana kiume leo waitoe Ethiopia

  Na Mwandishi EWetu, ADDIS ABABA
  NAHODHA wa Tanzania Bara, ‘Kilimanjaro Stars’ amesema kwamba watapigana ‘kufa na kupona’ kuhakikisha wanawatoa Ethiopia leo katika Ratiba Robo Fainali Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge.
  “Ni mchezo mgumu, kwa sababu wao wanacheza nyumbani na tumekwishaona jinsi wanavyopewa sapoti na mashabiki wa kwao. Kwa kweli utakuwa mtihani mgumu, lakini sisi tumejipanga,”amesema Bocco.
  Robo Fainali za CECAFA Challenge zinaanza leo katika Uwanja wa Taifa wa Addis Ababa, Ethiopia, mechi ya kwanza ikizikutanisha Uganda na Malawi na baadaye Tanzania Bara na Sudan. Hatua hii itahitimishwa kesho kwa michezo mingine miwili ya Robo Fainali, wa kwanza ukizikutanisha Sudan Kusini na Sudan na wa pili ukiwakutanisha Rwanda na Kenya.
  Bocco amesema wanaomba Mungu awajaalie washinde mchezo wa leo na kwenda Nusu Fainali, ili kurejesha imani ya Watanzania kwa timu zao za taifa.
  “Tunajua tuna deni kubwa kwa Watanzania, kwa kweli tutajitahidi sana tuweze kufanya vizuri ili wananchi warejeshe imani na timu yao,”amesema Bocco.
  Tanzania Bara na Ethiopia zote zimetoka Kundi A na mechi baina yao zilitoka sare ya 1-1, hivyo mchezo wa leo unatarajiwa kuwa mkali zaidi.
  Bara imepita kama mshindi wa kwanza wa Kundi A, wakati Ethiopia imepenya kwenye tundu la sindano kama mshindi wa tatu bora namba mbili, nyuma ya Sudan.
  Bara, Rwanda kutoka Kundi A, Uganda, Kenya kutoka Kundi B na Sudan Kusini na Malawi kutoka Kundi C hizo ndizo zimefuzu kwa kushika nafasi mbili za juu kwenye makundi yao. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BOCCO: HAWA WAHABESHI AMA ZAO, AMA ZETU LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top