• HABARI MPYA

  Jumatatu, Novemba 23, 2015

  MALAWI YAIPIGA SUDAN 2-1, SUDAN KUSINI YAWALAZA 2-0 DJIBOUTI

  MATOKEO NA RATIBA CHALLENGE 2015
  Novemba 21, 2015
  Burundi 1-0 Zanzibar 
  Ethiopia 0-1 Rwanda
  Novemba 22, 2015
  Somalia 4-0 Tanzania 
  Kenya 2-0 Uganda 
  Novemba 23, 2015
  Sudan Kusini 2-0 Djbouti 
  Sudan 1-2 Malawi
  Kesho; Novemba 24, 2015
  Zanzibar Vs Uganda 
  Rwanda Vs Tanzania 
  Malawi imeanza vyema michuano ya Challenge 2015

  WAALIKWA, Malawi ‘Flames’ wameanza vyema michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge baada ya kushinda mabao 2-1 dhidi ya Sudan katika mchezo wa Kundi C jioni ya leo nchini Ethiopia.
  The Flames walipata bao la kwanza dakika ya 15 kupitia kwa Chiukepo Msowoya, kabla ya Sudan  kusawazisha dakika tano baadaye kupitia kwa gwiji wake, Atahir El-Tahir.
  Dalitso Sailesi akaifungia Malawi bao la ushindi dakika ya 32 na tangu hapo walisota kusawazisha bila mafanikio, ikiwemo mkwaju wa penalti wa El-Tahir kuokolewa na kipa wa Malawi, Simplex Nthala.
  Katika mchezo uliotangulia, Sudan Kusini imeshinda 2-0 dhidi ya Djibouti mabao ya Bruno Martinez dakika ya 28 na Dominic Abuyo dakika ya 72.
  Ushindi huo unaifanya Sudan Kusini iongoze Kundi C kwa sasa. Malawi itamenyana na Djibouti katika mchezo ujao, wakati Sudan itacheza na Sudan Kusini.
  Michuano hiyo, inaendelea kesho kwa mchezo kati ya Zanzibar na Uganda Kundi B na Rwanda dhidi ya Tanzania Bara, Kundi A.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MALAWI YAIPIGA SUDAN 2-1, SUDAN KUSINI YAWALAZA 2-0 DJIBOUTI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top