• HABARI MPYA

  Jumapili, Novemba 22, 2015

  ETOILE NJE YA MLANGO WA CHUMBA ‘ALICHOFICHWA’ MWALI WA CAF

  TIMU ya Etoile du Sahel ya Tunisia imejisogeza karibu na taji la ubingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kulazimisha sare ya 1-1 ugenini jana.
  Etoile imetoka sare ya 1-1 na wenyeji Orlando Pirates Uwanja wa Orlando mjini Johannesburg, Afrika Kusini katika fainali ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika na sasa watatakiwa kwenda kushinda nyumbani kumaliza kazi.
  Pirates walianza kupata bao kupitia kwa mshambuliaji wao, Thamsanqa Gabuza dakika ya 36, kabla ya Sahel kusawazisha kupitia kwa Nahodha, Amar Jemal zikiwa zimebaki dakika tatu mchezo kumalizika.
  Kikosi cha Etoile du Sahel kilichocheza na Yanga SC Aprili 18, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

  Sasa hata sare ya 0-0 mjini Sousse, Tunisia wiki ijayo itawafanya Etoile waliyoitoa kwa mbinde Yanga SC ya Tanzania katika hatua ya 16 Bora washerehekee taji la Afrika. 
  Etoile ililazimisha sare ya 1-1 Dar es Salaam na kwenda kushinda 1-0 ‘kwa mbinde’ Suosse ili kusonga mbele.
  Aliyekuwa kiungo wa Yanga SC, Mrisho Ngassa ambaye sasa anachezea Free State Stars ya Afrika Kusini, akiwania mpira dhidi ya beki wa Etoile du Sahel ya Tunisia, Boughattas Zied katika mechi baina ya timu hizo Aprili 18, mwaka huu Uwanja wa Taifa
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ETOILE NJE YA MLANGO WA CHUMBA ‘ALICHOFICHWA’ MWALI WA CAF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top