• HABARI MPYA

  Jumatano, Novemba 25, 2015

  NAHODHA STARS JOHN BOCCO ASEMA; “TUNA DENI KUBWA KWA WATANZANIA”

  RATIBA KOMBE LA CHALLENGE 2015
  Leo; Novemba 25, 2015
  Kenya Vs Burundi 
  Somalia Vs Ethiopia 
  Malawi v Djibouti
  S. Sudan v Sudan
  Ijumaa Novemba 27, 2015
  Rwanda Vs Somalia
  Zanzibar Vs Kenya
  S. Sudan v Malawi
  Djibouti V Sudan
  Uganda Vs Burundi 
  Tanzania Vs Ethiopia
  Nahodha wa Kilimanjaro Stars, John Bocco amesema wana deni kwa Watanzania

  Na Mwandishi Wetu, ADDIS ABABA
  NAHODHA wa Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, John Raphael Bocco amesema kwamba wanafahamu wana deni kubwa kwa Watanzania, hivyo wataendelea kujitahidi wafanye vizuri katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge inayoendelea nchini Ethiopia.
  Kili Stars jana imekata tiketi ya Robo Fainali, baada ya kuichapa Rwanda mabao 2-1 katika mchezo wa Kundi A na kufikisha pointi sita baada ya mechi mbili, kutokana na awali kuifunga Somalia 4-0.
  Na sasa timu hiyo ya Kocha Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibaden’ itaingia kwenye mchezo wa mwisho dhidi ya wenyeji, Ethiopia kutafuta kuendelea kuongoza kundi hilo.
  “Tunamshukuru Mungu kwa matokeo haya, lakini hapa bado sana, tunajua tuna deni kubwa kwa Watanzania ambao wana kiu ya kufurahia mafanikio ya timu yao,”amesema Bocco.
  Mshambuliaji huyo wa Azam FC amesema kwamba wataendelea kujitahidi katika mechi zijazo waendelee kushinda hadi kutwaa ubingwa.
  “Tunajua Watanzania wamekata tamaa na timu yao, hususan kutokana na mwenendo mbaya katika siku za karibuni. Hilo ni deni letu sisi wachezaji na tutajitahidi tuwafariji,”amesema Bocco.
  Michuano ya CECAFA Challenge inaendelea leo kwa michezo minne ya makundi yote, Kenya dhidi ya Burundi Kundi B, Somalia dhidi ya Ethiopia Kundi A na ya Kundi C, kati ya Malawi na Djibouti na Sudan Kusini dhidi ya Sudan.
  Kesho ni mapumziko na keshokutwa mechi za makundi zitahitimishwa kwa michezo mine pia, Rwanda dhidi ya Somalia, Kili Stars na Ethiopia Kundi A, Zanzibar na Kenya, Uganda na Burundi Kundi B, Sudan Kusini na Malawi, Djibouti na Sudan Kundi C.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NAHODHA STARS JOHN BOCCO ASEMA; “TUNA DENI KUBWA KWA WATANZANIA” Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top