• HABARI MPYA

  Ijumaa, Novemba 27, 2015

  ZANZIBAR YAIBAMIZA KENYA 3-1 NA KUFUFUA MATUMAINI YA ROBO FAINALI

  MATOKEO NA RATIBA KOMBE LA CHALLENGE 2015
  Leo; Novemba 27, 2015
  Rwanda 3-0 Somalia
  Zanzibar 3-1 Kenya
  Sudan Kusini 2-0 Malawi
  Djibouti 0-4 Sudan
  Kesho; Novemba 28, 2015
  Uganda Vs Burundi 
  Tanzania Vs Ethiopia
  Zanzibar Heroes sasa yaweza kwenda Robo Fainali Challenge

  ZANZIBAR imeweka hai matumaini ya kwenda Robo Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge kama mmoja wa washindi watatu bora, baada ya kuifunga Kenya mabao 3-1 jioni ya leo nchini Ethiopia.
  Shukrani kwao wafungaji wa mabao hayo, Suleiman Kassim ‘Selembe’ mawili na Khamis Mcha ‘Vialli’ moja, wakati bao la Kenya limefungwa na Jacob Keli.
  Rwanda imeifunga 3-0 Somalia, mabao ya Jacques  Tuyisenge, Yussufu Habimana na Hegman Ngomirakiza, wakati Sudan Kusini imeifunga 2-0 Malawi, mabao ya James Joseph Saed na Bruno Martinez.
  Sudan imeifunga Djibouti 4-0, huku gwiji wake, Athar El Tahir akipiga hat-trick ya kwanza ya mashindano na bao lingine likifungwa na Faris Abdalla Mamoun.  
  Michuano hiyo itaendelea kwa mechi mbili kesho, kati ya Uganda na Burundi na Tanzania Bara dhidi ya Ethiopia zikihitimisha hatua ya makundi kuelekea Robo Fainali.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ZANZIBAR YAIBAMIZA KENYA 3-1 NA KUFUFUA MATUMAINI YA ROBO FAINALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top