• HABARI MPYA

  Jumanne, Novemba 24, 2015

  HATIMA YA ARSENAL LIGI YA MABINGWA NI LEO, MANCHESTER UTD, CHELSEA NAO VITANI ULAYA

  RATIBA MICHUANO YA LIGI YA MABINGWA ULAYA
  Leo Jumanne; Novemba 24, 2015
  Zenit St Petersburg Vs Valencia (Saa 1:00 usiku)
  BATE Borisov Vs Bayer 04 Leverkusen (Saa 1:00 usiku
  Maccabi Tel Aviv Vs Chelsea (Saa 3:45 usiku)
  Lyon Vs KAA Gent (Saa 3:45 usiku)
  FC Porto Vs Dynamo Kyiv (Saa 3:45 usiku)
  Bayern Munich Vs Olympiakos (Saa 3:45 usiku)
  Barcelona Vs Roma (Saa 3:45 usiku)
  Arsenal Vs Dinamo Zagreb (Saa 3:45 usiku)
  Kesho Jumatano; Novemba 25, 2015
  FC Astana Vs Benfica (Saa 3:45 usiku)
  CSKA Moscow Vs VfL Wolfsburg (Saa 1:00 usiku)
  Shakhtar Donetsk Vs Real Madrid (Saa 3:45 usiku)
  Manchester United Vs PSV (Saa 3:45 usiku)
  Malmo FF Vs Paris Saint-Germain (Saa 3:45 usiku)
  Juventus Vs Manchester City (Saa 3:45 usiku)
  Borussia Monchengladbach Vs Sevilla (Saa 3:45 usiku)
  Atletico Madrid Vs Galatasaray (Saa 3:45 usiku)
  Arsene Wenger anakabiliwa na mtihani mgumu leo Ligi ya Mabingwa Ulaya

  ARSENAL wanaikaribisha Dinamo Zagreb katika mchezo wa Kundi F, Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa leo Uwanja wa Emirates, London kuanzia Saa 3:45 kwa saa za Afrika Mashariki.
  Na timu ya Arsene Wenger inatakiwa lazima kushinda leo ili kujaribu kufufua matumaini ya kwenda hatua ya mtoano.
  Arsenal kwa sasa inashika nafasi ya tatu katika Kundi F, baada ya kuvuna pointi tatu tu katika mechi tatu za awali ilizocheza ikifungwa tatu na kushinda moja.
  Bayern Munich inaongoza kundi hilo kwa pointi zake tisa na mabao 10 zaidi ya Olympiacos yenye pointi tisa pia.
  Arsenal iwapo itashinda leo, itabidi iiombee mabaya Olympiacos ifungwe na Bayern Munich leo. Na pia katika mchezo wa mwisho, The Gunners iifunge Olympiacos na kumaliza nafasi ya pili katika kundi F. 
  Chelsea watasafiri kuifuata Maccabi Tel Aviv katika mchezo ambao wakishinda watajihakikishia kwenda hatua ya 16 Bora.
  Manchester United watakuwa wenyeji wa PSV kesho katika mchezo ambao wakishinda nao watakuwa tayari wametinga 16 Bora.
  Manchester City watakuwa wageni wa Juventus kesho katika mchezo ambao sana watakuwa wanawania kujihakikishia kumaliza kileleni mwa Kundi D, kwani kwa pointi zao tisa ni kama tayari wamefuzu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: HATIMA YA ARSENAL LIGI YA MABINGWA NI LEO, MANCHESTER UTD, CHELSEA NAO VITANI ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top