• HABARI MPYA

    Saturday, November 28, 2015

    MAN UNITED YAPOROMOKA ENGLAND REKODI YA VAN NISTERLOOY IKIVUNJWA LIGI KUU

    MATOKEO NA RATIBA LIGI KUU YA ENGLAND
    Leo Novemba 28, 2015  
    Leicester City 1-1 Manchester United
    Sunderland 2-0 Stoke City
    Manchester City 3-1 Southampton
    Bournemouth 3-3 Everton
    Crystal Palace 5-1 Newcastle United
    Aston Villa 2-3 Watford
    Kesho Novemba 29, 2015
    Tottenham Hotspur Vs Chelsea (Saa 9:00 Alasiri)
    West Ham Vs West Bromwich (Saa 11:05 jioni)
    Norwich City Vs Arsenal (Saa 1:15 usiku)
    Liverpool Vs Swansea City (Saa 1:15 usiku)
    Mshambuliaji wa Manchester United, Anthony Martial akimiliki mpira mbele ya kiungo wa Leicester City, Ngolo Kante usiku huu PICHA ZAIDI GONGA HAPA

    MANCHESTER United imepoteza nafasi ya kupanda kileleni mwa Ligi Kuu ya England, baada ya kutoa sare ya 1-1 na wenyeji, Leicester City Uwanja wa King Power usiku huu. 
    United inafikisha pointi 28 na kushuka kwa nafasi moja hadi ya tatu, nyumba ya Leicester City na Manchester City zenye pointi 29 kila moja, baada ya timu zote hizo kucheza mechi 14.
    Mshambuliaji wa Leicester, Jamie Vardy ameweka jina lake katika vitabu vya kumbukumbu za Ligi Kuu ya England baada ya kuifungia bao la kuongoza timu yake dakika ya 24.
    Mpachika mabao huyo amevunja rekodi ya gwiji wa Man United, Mholanzi Ruud van Nisterlooy kwa kuwa mchezaji wa kwanza kufunga katika mechi 11 mfululizo za Ligi Kuu.
    Kiungo Bastian Schweinsteiger aliisawazishia Manchester United dakika ya 46.

    Mshambuliaji wa Crystal Palace, Wilfried Zaha akiifungia timu yake katika ushindi wa 5-1 dhidi ya Newcastle United leo PICHA ZAIDI GONGA HAPA

    Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Sunderland imeshinda 2-0 dhidi ya Stoke City Uwanja wa Light, mabao ya Patrick van Aanholt dakika ya 82 na Duncan Watmore dakika ya 84.
    Manchester City imerejea kileleni kwa ushindi wa 3-1 dhidi ya Southampton, mabao yake yakifungwa na Kevin De Bruyne dakika ya tisa, Fabian Delph dakika ya 20 na Aleksandar Kolarov dakika ya 69, wakati la ‘Watakatifu’ limefungwa na Shane Long dakika ya 49 Uwanja wa Etihad.
    Bournemouth imetoa sare ya 3-3 na Everton, mabao yao yakifungwa na Adam Smith dakika ya 80 na Junior Stanislas mawili dakika ya 87 na 98, wakati ya wageni yamefungwa na Ramiro Funes Mori dakika ya 25, Romelu Lukaku dakika ya 36 na Ross Barkley dakika ya 95 Uwanja wa Vitality.
    Crystal Palace imeichapa 5-1 Newcastle United, mabao yake yakifungwa na James McArthur dakika ya 14, Yannick Bolasie dakika ya 17 na 47, Wilfried Zaha dakika ya 41 na James McArthur dakika ya 93, wakati la wageni limefungwa na Papiss Demba Cisse dakika ya 10 Uwanja wa Selhurst Park.

    Mshambuliaji wa Leicester, Vardy amevunja rekodi baada ya kufunga mfululizo katika mechi 11 za Ligi Kuu ya England 

    Watford imeshinda 3-2 ugenini dhidi ya Aston Villa Uwanja wa Villa Park, mabao yake yakifungwa na Odion Ighalo dakika ya 17, Alan Hutton aliyejifunga dakika ya 69 na Troy Deeney dakika ya 85, wakati ya wenyeji yamefungwa na Micah Richards dakika ya 41 na Jordan Ayew dakika ya 89.
    Ligi Kuu England itaendelea kesho kwa michezo minne, Tottenham Hotspur na Chelsea Uwanja wa White Hart Lane, West Ham United na West Bromwich Albion Uwanja wa Boleyn Ground, Norwich City na Arsenal Uwanja wa Carrow Road na Liverpool dhidi ya Swansea City Uwanja wa Anfield.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAN UNITED YAPOROMOKA ENGLAND REKODI YA VAN NISTERLOOY IKIVUNJWA LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top