• HABARI MPYA

  Jumanne, Septemba 29, 2015

  BARCELONA BILA MESSI KUWAVAA BAYER LEO LIGI YA MABINGWA ULAYA

  MECHI ZA LIGI YA MABINGWA LEO NA KESHO

  Jumanne Septemba 29, 2015

  Barcelona Vs Bayer 04 Leverkusen

  BATE Borisov Vs Roma

  FC PortoVs Chelsea

  Bayern Munich Vs Dinamo Zagreb

  Arsenal Vs Olympiakos

  Lyon Vs Valencia CF

  Maccabi Tel Aviv Vs Dynamo Kyiv

  Zenit St Petersburg Vs AA Gent

  Jumatano Septemba 30, 2015

  FC Astana v Galatasaray

  CSKA Moscow Vs PSV

  Juventus Vs Sevilla

  Borussia Monchengladbach Vs Manchester City

  Malmo FF Vs Real Madrid

  Manchester United Vs VfL Wolfsburg

  Atletico MadridVs Benfica

  Shakhtar Donetsk Vs Paris Saint-Germain

  Barcelona watamkosa Lionel Messi leo wakiikaribisha Bayer Leverkusen Uwanja wa Camp Nou


  HATUA ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, inaendelea leo na kesho, huku mabingwa watetezi, Barcelona wakiikaribisha Bayer 04 Leverkusen Uwanja wa Camp Nou mjini Barcelona, Hispania.

  Katika mchezo huo, Barcelona watamkosa nyota wake, Lionel Messi aliyeumia mwishoni mwa wiki katika mchezo wa La Liga ikishinda 2-1 dhidi ya Las Palmas Barcelona, lakini hapana shaka Neymar na Luis Suarez watawabeba wababe hao wa Katalunya.

  BATE Borisov watakuwa wenyeji wa Roma Uwanja wa Borisov Arena, Chelsea wataifuata FC Porto Uwanja wa DragaoBayern Munchen wataikaribisha Dinamo Zagreb Uwanja wa Allianz Arena, Arsenal wataikaribisha Olympiakos Uwanja wa Emirates, Lyon wataikaribisha Valencia Uwanja wa Stade de Gerland, Maccabi Tel Aviv wataikaribisha Dynamo Kyiv Uwanja wa Bloomfield na Zenit St Petersburg wataikaribisha KAA Gent  Uwanja wa Petrovski.

  Messi aliumia mwishoni mwa wiki katika mchezo wa La Liga ikishinda 2-1 dhidi ya Las Palmas Barcelona


  Michuano hiyo itaendelea kesho FC Astana ikiikaribisha Galatasaray Uwanja wa Astana Arena, CSKA Moscow ikiikaribisha PSV Uwanja wa Arena Khimki, Juventus ikiikaribisha Sevilla Uwanja wa Juve, Borussia Monchengladbach ikiwakaribisha Manchester City Uwanja wa Borussia-Park, Malmo FF ikiwakaribisha Real Madrid Uwanja wa Swedbank, Manchester United ikiwakaribisha VfL Wolfsburg Uwanja wa Old Trafford Atletico de Madrid ikiwakaribisha Benfica Uwanja wa Vicente Calderon na Shakhtar Donetsk wakiwakaribisha Paris Saint-Germain Uwanja wa Lviv. 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BARCELONA BILA MESSI KUWAVAA BAYER LEO LIGI YA MABINGWA ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top