• HABARI MPYA

  Jumamosi, Septemba 26, 2015

  SANCHEZ APIGA HAT TRICK, ARSENAL YAICHAPA 5-2 LEICESTER

  ARSENAL imeibuka na ushindi wa mabao 5-2 ugenii dhidi ya Leicester katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni ya leo.
  Jamie Vardy alianza kuifungia Leicester dakika ya 13 Uwanja wa King Power, kabla ya Theo Walcott kuisawazishia The Gunners dakika tatu baadaye akimtungua kipa Kasper Schmeichel.
  Alexis Sanchez akafunga mabao matatu katika dakika za 33, 57 na 81 kabla ya Vardy kuifungia tena Leicester dakika ya 89 na Olivier Giroud akafunga la nne dakika ya 90. 
  Kikosi cha Leicester kilikuwa; Schmeichel, de Laet, Huth, Morgan, Schlupp, Mahrez, Kante, Drinkwater/Kramaric dk78, Albrighton/Ulloa dk64, Okazaki/King dk45 na Vardy. 
  Arsenal; Cech, Bellerin, Mertesacker, Koscielny, Monreal, Flamini/Arteta dk21, Cazorla, Ramsey/Oxlade-Chamberlain dk77, Ozil, Sanchez na Walcott/Giroud dk80.
  Mshambuliaji wa Arsenal, Alexis Sanchez (katikati) akishangilia baada ya kuifungia hat trick Arsenal dhidi ya Leicester leo PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SANCHEZ APIGA HAT TRICK, ARSENAL YAICHAPA 5-2 LEICESTER Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top