• HABARI MPYA

  Jumapili, Septemba 20, 2015

  ULIMWENGU APIGA MBILI MAZEMBE IKIUA 4-1 DRC, KIKOSI CHAWAFUATA MAPEMA MERREIKH

  Thomas Ulimwengu juzi amefunga mabao mawili Mazembe ikishinda 4-1
  MSHAMBULIAJI Mtanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu juzi alifunga mabao mawili katika ushindi wa TP Mazembe wa 4-1 dhidi ya New Soger Ligi Kuu ya DRC na jana asubuhi kikosi cha timu kimeelekea Sudan.
  Saa kadhaa baada ya ushindi huo wa 4-1, Ulimwengu aliongoza msafara wa furaha kwa safari ya Sudan kwenda kumenyana na wenyeji, El Merreikh katika Nusu Fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
  Septemba 26, Mazembe watashuka Uwanja wa Merreikh mjini Khartoum kumenyana na wenyeji wao katika Nusu Fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa na timu hiyo ya Lubumbashi imeamua kuwahi Sudan ili kuzoea hali ya hewa.
  Mbwana Samatta akifurahia baada ya kufunga mabao matatu katikaushindi wa 5-0 dhidi ya Moghreb

  Shirikisho la Soka Kongo limefuta mchezo wa Ligi Kuu wa Mazembe na Pacific Ocean Mbuji-Mayi uliokuwa ufanyike Jumatano ili mabingwa hao mara nne Afrika wawahi Sudan kwa maandalizi mazuri.
  Na Mazemba inatua Khartoum huku washambuliaji wote wa Tanzania wanaochezea timu hiyo, Ulimwengu na Mbwana Ally Samatta wakiwa katika kiwango cha juu.
  Samatta alifunga mabao matatu peke yake katika mchezo wa mwisho wa Kundi A Ligi ya Mabingwa Mazembe ikishinda 5-0 dhidi ya Moghreb Tetouan ya Morocco wiki iliyopita mjini Lubumashi.
  Wachezaji wa TP Mazembe, Gladson Awako na Yaw Frimpong wakiwa kwende ndege jana kwa safari ya Sudan
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ULIMWENGU APIGA MBILI MAZEMBE IKIUA 4-1 DRC, KIKOSI CHAWAFUATA MAPEMA MERREIKH Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top