| Timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania, Twiga Stars imelazimisha sare ya 0-0 na Afrika Kusini katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Kintele mjini Brazaville, Kongo. Twiga Stars imecheza mechi hiyo baada ya kutolewa katika Michezo ya Afrika inayoendelea Kongo-Brazaville kufuatia kushika nafasi Kundi A nyuma ya Ivory Coast na Nigeria na mbee ya wenyeji Kongo. Twiga inatarajiwa kurejea nchni Ijumaa. Pichani ni kikosi cha Twiga Stars katika mashindano hayo |
0 comments:
Post a Comment