• HABARI MPYA

  Jumamosi, Septemba 26, 2015

  NGASSA AWAKOSAKOSA BIDVEST WITS, ALIPIGA BONGE LA ‘FREE KICK’ LIKAOKOLEWA LINAKWENDA NYAVUNI

  KIUNGO mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mrisho Khalfan Ngassa leo amepiga mpira wa dhabu uliokaribia kuipa bao Free State Stars ikitoa sare ya 0-0 na Bidvest Wits katika Ligi Kuu ya ABSA Afrika Kusini.
  Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Goble Park mjini Bethelehem, Ngassa alipiga mpira huo dakika ya sita baada ya kuanza kipindi cha pili na kuokolewa ukiwa unaelekea kutinga nyavuni.
  Mrisho Ngassa (kulia) leo amewakosa bao Bidvest Wits

  Haikuwa bahati yao leo Ea Lla Koto wakicheza nyumbani, kwani walikosa mabao zaidi ya matatu ya wazi.
  Kikosi cha Stars kilikuwa: Diakite, Mashego, Shabalala, Sankara, Thlone, Somaeb/Rakoti dk46, Masehe, Mohomi/Sekola dk46, Venter, Ngassa na Fileccia.
  Wits: Josephs, Nhlapo, Mkhwanazi, Hlatshwayo, Bhasera, Lecki, Ngcepe/Bright dk61, Faty/Klate dk90+1, Shongwe/Gome dk63, Ntshangase na Lupeta.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NGASSA AWAKOSAKOSA BIDVEST WITS, ALIPIGA BONGE LA ‘FREE KICK’ LIKAOKOLEWA LINAKWENDA NYAVUNI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top