• HABARI MPYA

    Tuesday, September 29, 2015

    REFA NKONGO KUCHUNGUZWA KWA TUHUMA ZA 'KUWAUMA' SIMBA SC WAKIPIGWA 2-0 NA YANGA

    KAMATI ya Uendeshaji wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara imesema itautazama tena mchezo wa ligi hiyo kati ya Simba SC na Yanga SC uliofanyika Jumamosi, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ili ili kutathmini uchezeshaji wa refa, Israle Mujuni Nkongo.
    Hiyo inafuatia malalamiko ya Simba SC iliyofungwa 2-0 kwamba Nkongo aliwaonea katika uchezaji wake, kiasi cha kufikiwa hadi kuwatukana wachezaji wao walipojaribu kulalamika.
    Pamoja na hayo, Kamati hiyo imeipiga faini Simba SC kwa kitendo cha wapenzi na mashabiki wake kuwashambulia waamuzi baada ya mchezo huo kwa kuwarushia chupa za maji ambazo nyingine ziliwakosa waamuzi na kumpata kocha wa Yanga Hans Van Pluijm.
    Refa Israel Nkongo (wa tatu kulia) atachunguzwa kutokana na tuhuma za Simba SC

    Katika kikao chake cha leo kupitia ripoti mbalimbali za michezo iliyochezwa mwishoni mwa wiki ya Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza, Kamati hiyo imemfungia beki Juma Nyoso wa Mbeya City kwa miaka miwili na kumpiga faini ya Sh Milioni 2, kufutia kitendo cha udhalilishaji alichomfanyia mshambuliaji wa Azam FC, John Bocco.
    Aidha, Yanga SC, imepigwa faini ya Sh 500,000 kufutia wachezaji wake watano, Salum Telela, Mbuyu Twite, Malimi Busungu, Ali Mustafa 'Barthez' na Donald Ngoma. kuonyeshwa kadi za njano katika mchezo dhidi ya Simba SC. Kwa mujibu wa kanunu namba 42 (11) timu ambayo wachezaji wake watapata kadi zaidi ya tabo katika mchezo mmoja itapigwa faini ya shilingi laki tano.
    Yanga SC pia imepigwa faini nyingine ya Sh 500,000 kufutia wachezaji wake kwenda kushangilia upande wa Simba SC mara baada ya mchezo kumalizika.
    Taarifa ya TFF jioni hii, imesema kwamba mchezo namba 26 wa VPL kati ya Coastal Union na Mwadui uliofanyika kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga. Chumba cha Coastal Union kilikuwa na harufu kali sana. Baadhi ya mashabiki wa Coastal Union waliokuwa nyuma ya goli la upande wa kaskazini walitoa  lugha ya matusi kwa waamuzi na kutishia kuwapiga na pia walimrushia mawe mwamuzi msaidizi wa pili Shafii Mohamed na jiwe moja lilimpiga mgongoni na kumjeruhi kidogo mwamuzi na aliomba msaada wa jeshi la polisi kutuliza ghasia, mchezo ulisimama kwa dakika 3.
    Kwa mujibu wa kanuni namba 42 (1) ya udhibiti wa wachezaji Coastal Union itatozwa faini ya Tsh 500,000/=
    Mchezo namba 22 wa VPL kati ya Mtibwa Sugar na Ndanda uliofanyika kwenye uwanja wa Manungu, Turiani. Ndanda hawakuleta watu wa kutosha kwenye pre match meeting hivyo wanapigwa faini ya shilingi laki mbili (200,000/=)
    Mchezo namba 23 wa VPL kati ya Simba SC na Kagera Sugar uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa, Dar es salaam. Simba walikuwa na wajumbe watatu na Kagera Sugar walikuwa na mtu mmoja tu tena hakuja na vifaa. Timu zote zimepigwa faini ya shilingi laki mbili (200,000).
    Mchezo namba 17 wa VPL kati ya Stand united na African Sports kocha wa Stand United alitolewa nje ya eneo la ufundi kwa kutoheshimu taratibu za eneo hilo na pia alikataa kuongea na vyombo vya habari kwa hiyo kwa mujibu wa kanuni namba 40 (11) anafungiwa kukaa kwenye benchi la ufundi kwa mechi mbili na faini ya sh 500,000/= kwa kila kosa jumla 1,000,000/=.
    Friends Rangers na KMC Mechi Na 8 Kundi A iliyofanyika uwanja wa Karume 27.9.2015. Timu ya KMC ya kinondoni ilifanya mabadiliko kwa kuingiza wachezaji 4 ambao ni kinyume cha kanuni. 
    Kwa mujibu wa taarifa ya mwamuzi wachezaji waliofanyiwa mabadiliko ni Frank Mashoto badala ya Kudra Omar, Kamongo Morris badala ya Mrisho Simon, Mfanyeje Mussa badala ya Kabange Mgunda na Sultani Kasiras badala ya Adam Said.

    Kwa mujibu wa kanuni namba 14 (25) KMC imepoteza mechi na kupigwa faini ya Tsh 200,000/=. Mwamuzi wa akiba anafutwa kuchezesha ligi msimu huu na mwamuzi wa kati anapewa onyo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: REFA NKONGO KUCHUNGUZWA KWA TUHUMA ZA 'KUWAUMA' SIMBA SC WAKIPIGWA 2-0 NA YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top