• HABARI MPYA

  Jumamosi, Septemba 26, 2015

  GABRIEL WA ARSENAL ANUSURIKA KUFUNGIWA MECHI TATU, SASA ATAKOSA MCHEZO MMOJA TU

  BEKI wa Arsenal, Gabriel amenusurika kufungiwa mechi tatu na badala yake kusimamishwa kwa mchezo mmoja tu na Chama cha Soka England baada ya kukiri kosa.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 aligombana na Diego Costa na kuonyesha kadi nyekundu Chelsea ikiilaza The Gunners mabao 2-0 Uwanja wa Stamford Bridge, London katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.
  FA imesema kwamba imekubakiana na malalamiko ya Arsenal dhidi ya uamuzi wa refa Mike Dean na kuondoa adhabu ya mechi tatu, lakini beki huyo Mbrazil hajaepuka adhabu. 
  Beki wa Arsenal, Gabriel (katikati) ameepuka adhabu ya mechi tatu baada ya kukatiwa rufaa FA PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: GABRIEL WA ARSENAL ANUSURIKA KUFUNGIWA MECHI TATU, SASA ATAKOSA MCHEZO MMOJA TU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top