• HABARI MPYA

    Tuesday, September 22, 2015

    LIGI KUU YA WANAWAKE TANZANIA KUANZA MWAKANI

    KATIKA harakati za kuinua kiwango cha soka ya wanawake nchini, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limepanga kuendesha Ligi Kuu ya wanawake nchini kuanzia mwakani.
    Ofisa Habari wa TFF, Baraka Kizuguto amesema kwamba TFF imeviagiza vyama vya mikoa kuendesha mashindano ya Ligi ya Mabingwa wa mikoa kwa wanawake haraka iwezekanavyo kabla ya Desemba 31, mwaka huu ili kupata timu za kushiriki Ligi Kuu.
    "Kila chama cha mkoa cha mpira wa miguu nchini kinapaswa kuwasilisha jina la bingwa wa mkoa mwishoni wa mwezi Disemba mwaka huu, kwa ajili ya maandalizi ya Ligi ya Taifa ya Wanawake inayotarajiwa kufanyika mwakani,"amesema Kizuguto.
    Ligi ya Taifa ya Wanawake inatarajiwa kuanza mapema mwakani baada ya kupatikana mabingwa wa mikoa 27 nchini ikijumuisha mkoa wa Dar es salaam utakaokuwa na timu tatu za Ilala, Kinondoni na Temeke.
    Jumla ya timu 10 zinatarajiwa kupanda Ligi Kuu ya Wanawake Taifa baada ya timu za mikoa 27 kucheza ligi ya mabingwa na kupata timu 10 zitakazoanza kwenye ligi hiyo ya wanawake mwakani.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: LIGI KUU YA WANAWAKE TANZANIA KUANZA MWAKANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top