• HABARI MPYA

  Jumanne, Septemba 22, 2015

  AZAM FC WAREJEA DAR KUISUBIRI MBEYA CITY, PATASHIKA LITAKUWA CHAMAZI JUMAPILI HII

  MECHI ZIJAZO LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA
  Jumamosi Septemba 26, 2015
  Simba SC Vs Yanga SC
  Coastal Union Vs Mwadui FC
  Prisons FC Vs Mgambo JKT
  JKT Ruvu Vs Stand United
  Mtibwa Sugar Vs Majimaji FC
  Kagera Sugar Vs Toto Africans
  Septemba 27, 2015
  African Sports Vs Ndanda FC
  Azam FC Vs Mbeya City 
  Azam FC watakuwa wenyeji wa Mbeya City katika mchezo ujao wa Ligi Kuu 

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  AZAM FC imerejea jana usiku Dar es Salaam kutoka Shinyanga ambako ilifanikiwa kuvuna pointi sita katika mechi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Stand United na 1-0 dhidi ya Mwadui FC, Azam FC imetua kwa ndege usiku wa jana Dar es Salaam kwa maandalizi ya mchezo ujao dhidi ya Mbeya City.
  Mabingwa hao wa Afrika Mashariki na Kati watakuwa wenyeji wa Mbeya City katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Azam FC imeshinda mechi zote tatu za mwanzo za Ligi Kuu, dhidi ya Prisons 2-1 Chamazi na hizo za Shinyanga, ikiwa inababana mbavu na vigogo, Simba na Yanga SC kileleni.
  Mechi za Azam FC inayodhaminiwa na benki ya NMB na Mbeya City inayodhaminiwa na RB Battery za Bin Slum Company Limited, zimekuwa kali na za kusisimua popote zinapokutana timu hizo, iwe Mbeya au Chamazi na Jumapili inatarajiwa patashika nyingine.

  MSIMAMO WA LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA
  # TimuPWDLFADPtsMechi zilizopita 
  1Previous rank: 16330091+89WWW
  2Previous rank: 12330061+59WWW
  3Previous rank: 2330051+49WWW
  4Previous rank: 8330052+39WWW
  5Previous rank: 6320121+16LWW
  6Previous rank: 10311133+04LWD
  7Previous rank: 15311122+04DLW
  8Previous rank: 4311123-14WLD
  9Previous rank: 7310232+13LWL
  10Previous rank: 9310222+03LWL
  11Previous rank: 13310223-13WLL
  12Previous rank: 5310224-23LLW
  13Previous rank: 14310225-33WLL
  14Previous rank: 3301203-31DLL
  15Previous rank: 1300305-50LLL
  16Previous rank: 11300318-70LLL
  Ligi Kuu inayoonyeshwa moja kwa moja na Azam TV itaendelea Jumamosi ya Septemba 26 kwa mchezo kati ya mahasimu Simba SC na Yanga SC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Coastal Union na Mwadui FC Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, Prisons FC na Mgambo JKT Uwanja wa Sokoine, Mbeya, JKT Ruvu na Stand United Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, Mtibwa Sugar na Majimaji FC Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro, Kagera Sugar na Toto Africans wakati Jumapili African Sports watakuwa wenyeji wa Ndanda FC Mkwakwani na Azam FC na Mbeya City Chamazi. 
  Baada ya raundi tatu za awali, mabingwa watetezi Yanga SC wanaongoza Ligi Kuu kwa wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa, kufuatia kufungana kwa pointi na Simba na Azam FC.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM FC WAREJEA DAR KUISUBIRI MBEYA CITY, PATASHIKA LITAKUWA CHAMAZI JUMAPILI HII Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top