• HABARI MPYA

  Jumatatu, Septemba 21, 2015

  SIMBA SC NA KAGERA SUGAR KATIKA PICHA JANA UWAJA WA TAIFA

  Mshambuliaji wa Simba SC, Hamisi Kiiza ''Diego' (kulia) akimtoka beki wa Kagera Sugar, Job Ibrahim (kushoto) katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Simba SC ilishinda 3-1, Kiiza akifunga mabao yote.
  Beki wa Kagera Sugar, Said Hassan akinyoosha mguu kumzuia beki wa Simba SC, Emery Nimubona
  Kiungo wa Simba SC, Peter Mwalyanzi (wa pili kulia) akimuacha chini beki wa Kagera Sugar, Salum Kanoni huku Deogratius Julius akiendelea kumfukuza na kushoto kabisa ni kipa Agathony Anthony
  Kiungo wa Simba SC, Said Ndemla (kushoto) akiwatoka kwa ustadi wa hali ya juu wachezaji wa Kagera Sugar, George Kavila na Paul Ngalyoma kushoto
  Hamisi Kiiza akiwa amemuangukia kifuani Salum Kanoni kwenye boksi la Kagera Sugar
  Mshambuliaji wa Simba SC, Ibrahim Hajib akitafuta maarifa ya kumtoka Deo Julius wa Kagera

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA SC NA KAGERA SUGAR KATIKA PICHA JANA UWAJA WA TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top