• HABARI MPYA

  Alhamisi, Septemba 24, 2015

  SHERMAN AENDELEA KUNG’ARA AFRIKA KUSINI, TIMU YAKE YASHINDA 2-1 UGENINI

  MSHAMBULIAJI wa zamani wa Yanga SC, Mliberia Kpah Sherman jana amecheza kwa dakika 63 timu yake mpya, Mpumalanga Black Aces ikiendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya ABSA Afrika Kusini.
  Aces imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 ugenini jana usiku, shukrani kwake mkongwe Collins Mbesuma aliyefunga mabao yote hayo dhidi ya Golden Arrows Uwanja wa King Zwelithini mjini Durban.
  Sherman alianza katika mchezo huo kabla ya kumpisha Aubrey Modiba dakika ya 63 wakati huo tayari Aces inaongoza 2-1.
  Deon Hotto alianza kuwafungia Arrows dakika ya 13 akimalizia pasi ya Gladwin Shitolo, lakini Mbesuma akasawazisha dakika ya 32 na kufunga la pili dakika ya 49.
  Sherman ametua Aces mwezi uliopita kutoka Yanga SC ambako alicheza kwa nusu msimu huu kabla ya kuamua kuondoka baada ya kuona mambo hayamuendi vizuri.
  Mechi nyingine za Ligi Kuu ya ABSA jana, Kaizer Chiefs imelazimishwa sare ya  1-1 University of Pretoria Uwanja wa FNB, bao lao likifungwa na Bernard Parker dakika ya 25 kabla ya  Tebogo Monyai kuwasawazishia wapinzani wao dakika ya 70, wakati Mamelodi Sundowns imeshinda 3-2 dhidi ya Ajax Cape Town, mabao yake yakifungwa na Teko Modise dakika ya 20, Cecil Lolo akijifunga dakika ya 42 na Anthony Laffor dakika ya 90, ya wapinzani wao yakifungwa na Bantu Mzwakali dakika ya 36 na Nathan Paulse kwa penalti dakika ya 46 Uwanja wa Lucas Moripe.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SHERMAN AENDELEA KUNG’ARA AFRIKA KUSINI, TIMU YAKE YASHINDA 2-1 UGENINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top