• HABARI MPYA

  Jumanne, Septemba 29, 2015

  TFF YAMFUNGIA NYOSSO MIAKA MIWILI NA FAINI MILIONI 2, YANGA NAO WAKAMULIWA MAMILIONI

  KAMATI ya uendeshaji wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara iliyokutana leo kupitia ripoti mbalimbali za michezo iliyochezwa ya ligi hiyo na Ligi Daraja la Kwanza ya Azam TV, imemfungia Nahodha wa Juma Said Nyoso wa Mbeya City kwa miaka miwili na kumtoza faini ya Sh Milioni 2, kufutia kitendo cha udhalilishaji alichomfanyia Nahodha wa Azam FC John Raphael Bocco.
  Nyoso alifanya kitendo hicho katika mchezo no namba 32 wa VPL kati ya Azam FC na Mbeya City uliofanyika kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam, hiyo ikiwa mara ya nne na mara pili kwa mwaka kufanya vitendo hivyo vya utovu wa nidhamukwenye michezo ya Ligi Kuu.
  Klabu ya Yanga SC imepigwa faini ya Sh 500,000 kufutia wachezaji wake watano kuonyeshwa kadi za njano katika mchezo dhidi ya Simba SC Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
  Kwa mujibu wa kanunu namba 42 (11) timu ambayo wachezaji wake watapata kadi zaidi ya tabo katika mchezo mmoja itapigwa faini ya shilingi laki tano. Wachezaji wa Yanga SC waliopata kadi za njano siku hiyo Salum Telela, Donald Ngoma, Malimi Busungu, Ali Mustafa na Mbuyu Twite.
  Aidha, Yanga imepigwa faini nyingine ya Sh 500,000 kufutia wachezaji wake kwenda kushangilia upande wa mashabiki wa Simba SC mara baada ya mchezo kumalizika.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TFF YAMFUNGIA NYOSSO MIAKA MIWILI NA FAINI MILIONI 2, YANGA NAO WAKAMULIWA MAMILIONI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top