• HABARI MPYA

  Jumatatu, Septemba 28, 2015

  NGASSA AOMBEWA UDHURU TAIFA STARS, MOROCCO ATAJA KIKOSI CHA KUIVAA MALAWI KUFUZU KOMBE LA DUNIA OKTOBA 9 DAR

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  KOCHA Msaidizi wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Hemed Morroco leo ametaja kikosi kwa ajili ya mchezo dhidi ya Malawi mwezi ujao, lakini mshambuliaji Mrisho Khafan Ngassa ameombewa udhuru.
  Free State Stars ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini imemuombea udhuru Mrisho Ngassa achelewe kidogo kujiunga na kambi ya maandalizi ya mchezo huo.
  Free State imewaandikia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuomba Ngassa ajiunge na kambi ya Stars baada ya Oktoba 4, akimaliza kuichezea klabu hiyo katika mchezo wa Kombe la Telkom Knockout dhidi ya Bidvest Wits Oktoba 3.   
  Morocco aliyetaja kikosi hicho badala ya bosi wake, Charles Boniface Mkwasa ambaye amekwenda Iringa kwenye msiba wa mama mkwe, amesema kikosi kitaingia kambini, Oktoba 1.
  Mrisho Ngassa (kulia) ameombewa udhuru na klabu yake kuchelewa kujiunga na kambi ya Taifa Stars kwa maandalizi ya mchezo dhidi ya Malawi

  Taifa Stars inatarajiwa kumenyana na Malawi Oktoba 9, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia 2018.
  Kikosi hicho kinaundwa na makipa; Aishi Manula (Azam FC), Ally Mustafa ‘Barthez’ (Yanga SC) na Said Mohammed (Mtibwa Sugar), mabeki; Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ (Simba SC), Juma Abdul (Yanga SC), Shomary Kapombe (Azam FC), Mwinyi Mngwali (Yanga SC), Hassan Isihaka (Simba SC), Kelvin Yondan (Yanga SC)na Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ (Yanga SC).
  Viungo ni Himid Mao (Azam FC), Said Ndemla (Simba SC), Salum Telela (Yanga SC), Frank Domayo (Azam FC), Mudathir Yahya (Azam FC), Simon Msuva (Yanga SC) na Deus Kaseke (Yanga SC), wakati washambuliaji ni Rashid Mandawa (Mwadui FC), John Bocco (Azam FC), Mrisho Ngassa (Free State Stars, Afrika Kusini), Mbwana Samatta (TP Mazembe, DRC), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC) na Farid Mussa (Azam FC).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NGASSA AOMBEWA UDHURU TAIFA STARS, MOROCCO ATAJA KIKOSI CHA KUIVAA MALAWI KUFUZU KOMBE LA DUNIA OKTOBA 9 DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top