• HABARI MPYA

  Jumapili, Septemba 20, 2015

  ANTHONY MARTIAL APIGA MBILI MAN UNITED YAICHAPA SOUTHAMPTON 3-2 ENGLAND

  MANCHESTER United imeshinda mabao 3-2 ugenini dhidi ya Southampton katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni ya leo.
  Graziano Pelle alianza kuwafungia wenyeji dakika ya 13 akiuwahi mpira uliorudi baada ya kazi nzuri ya Sadio Mane kuokolewa, lakini Anthony Martial akawasazishia Mashetani Wekundu dakika ya 34 na kufunga la pili dakika ya 50.
  Juan Mata akaifungia Man United bao la tatu dakika ya 68 baada ya kuuwahi mpira uliogonga mwamba na kurudi kufuatia shuti la Memphis Depay- na Pelle akaifungia Southampton bao la pili dakikaya 86.
  Timu ya Louis van Gaal inapanda nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England ikizidiwa pointi mbili tu na vinara, Manchester City. 
  Kikosi cha Southampton kilikuwa; Stekelenburg, Yoshida, Fonte, van Dijk, Targett/Martina dk46, Romeu/S Davis dk56, Wanyama, Ward-Prowse/Long dk76, Tadic, Mane na Pelle. 
  Manchester United; De Gea, Darmian/Valencia dk46, Smalling, Blind, Rojo/McNair dk69, Carrick/Schweinsteiger dk60, Schneiderlin, Mata, Rooney, Depay na Martial.
  Anthony Martial (kulia) akishangilia baada ya kuifungia Manchester United mabao mawili. Kushoto ni Juan Mata aliyefunga moja katika ushindi wa 3-2 PICHA ZAIDI GONGA HAPA\
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ANTHONY MARTIAL APIGA MBILI MAN UNITED YAICHAPA SOUTHAMPTON 3-2 ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top