• HABARI MPYA

  Jumapili, Septemba 20, 2015

  MINZIRO: NIKO TAYARI KUWAJIBIKA, WACHEZAJI WAMENIANGUSHA

  Kocha wa JKT Ruvu, Freddy Felix MInziro amesema kwamba yuko tayari kuwajibika kwa makosa ya wachezaji wake

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  KOCHA wa JKT Ruvu ya Pwani, Freddy Felix Minziro amesema kwamba yuko tayari kuwajibika kwa matokeo mabaya katika timu, lakini atakuwa anabeba msalaba kwa ajili ya wachezaji.
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS-ONLINE jana, Minziro amesema kwamba wachezaji wamemuangusha kwa kufanya makosa ya kizembe mechi zote tatu za mwanzo ambazio timu imepoteza katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  “Mimi ni kocha mzoefu ambaye wengi wanajua na kazi yangu inajulikana. Kama si kocha mzuri watu wanajua, kama ni kocha mzuri, watu wanajua. Timu hii mimi kama mwalimu nimefanya kila kitu katika maandalizi,”.
  “Tumefanya vizuri katika mechi za kujipima nguvu, lakini tunaanza mashindano, matokeo yanakuwa hivi, yaani huelewei wachezaji wanafanya nini. Lakini nitaendelea kupambana hali iwe shwari,”alisema.
  Pamoja na hayo beki huyo wa zamani wa Yanga SC, amesema atakuwa tayari kuwajibika iwapo atatakiwa kufanya hivyo na uongozi wa timu, kwani hiyo ni kawaida kwa makocha.
  “Siku zote makocha ndiyo wanabebeshwa misalaba, basi nami nikitakiwa kufanya hivyo, hakuna shinda, nitapumzika,”alisema.
  Minziro (kushoto) akiwa na kocha wa Yanga SC, Mholanzi, Hans van der Pluijm katika mkutano wa baada ya mechi jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

  JKT Ruvu jana imefungwa mechi ya tatu mfululizo ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kuchapwa mabao 4-1 na Yanga SC Dar es Salaam, ikitoka kufungwa 3-0 na Mbeya City na 1-0 na Majimaji mjini Songea.
  JKT Ruvu watashuka tena dimbani Septemba 26, mwaka huu kumenyana na Stand United ya Shinyanga Uwanja wa Karume, Dar es Salaam mchezo ambao watatakiwa lazima washinde ili kurejesha amani jeshini. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MINZIRO: NIKO TAYARI KUWAJIBIKA, WACHEZAJI WAMENIANGUSHA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top