• HABARI MPYA

  Jumatatu, Septemba 21, 2015

  KIUNGO FUNDI WA MTIBWA SUGAR AITWA MAMELODI SUNDWONS KUJARIBU BAHATI

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  KIUNGO wa Mtibwa Sugar ya Morogoro, Ismail Aidan Mwesa (pichani kushoto) amekwenda Afrika Kusini kufanya majaribio ya kujiunga na klabu ya Mamelodi Sundowns ya huko, imeelezwa.
  Meneja wa mchezaji huyo, Kabole Kahungwa ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, mchezaji huyo aliondoka mwishoni mwa wiki na atakuwa huko hadi wiki ijayo.
  Akielezea namna mchezaji huyo alivyopata nafasi hiyo, Kahungwa alisema kwamba walipeleka video za mchezaji huyo kwa wahusika wa masuala ya vipaji wa Mamelodi ambao baada ya kuvutiwa nazo, wakaleta mwaliko.
  “Nina imani sana na huyu kijana, kwa sababu ana kipaji cha hali ya juu. Muda wote alikuwa anacheza timu ya vijana ya Mtibwa, kama kupandishwa ilikuwa apandishwe msimu huu,”amesema Kabole.
  Kinda huyo aliyewahi kuchezea timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, anatarajiwa kuanza majaribio yake leo Afrika Kusini.   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KIUNGO FUNDI WA MTIBWA SUGAR AITWA MAMELODI SUNDWONS KUJARIBU BAHATI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top