• HABARI MPYA

  Ijumaa, Septemba 25, 2015

  KLITSCHKO AJITOA PAMBANO NA TYSON AKIDAI KUUMIA MAZOEZINI

  BONDIA Tyson Fury 'amemuwakia' mpinzani wake Wladimir Klitschko baada ya kujitoa kwenye pambano baina yao la ndondi za kulipwa uzito wa juu.
  Mbabe wa Ukraine ameumia msuli wa nyuma wa mguu mazoezini zikiwa ni wiki nne kabla ya pambano lake na Fury Oktoba 24, mwaka huu.
  Fury amemuambia Klitschko kupitia mitandao ya kijamii kwamba kukimbia siyo suluhisho. 
  Wladimir Klitschko (kushoto) amelazimika kujitoa katika pambano na Tyson Fury baada ya kuumia
  Promota wa Fury, Mick Hennessy amesema kwamba mazungumzo yamekwishaanza juu ya kulipanga upya pambano hilo na tarehe mpya itakuwa mwishoni mwa Novemba na litafanyika katika ukumbi ule ule, Esprit Arena mjini Dusseldorf, Ujerumani.
  Fury aliyekuwa mwenye kujiamini katikati ya wiki wakati wa kutangazwa kwa pambano lake na Klitschko, ambaye ni bingwa wa mataji ya dunia ya WBA, WBA na IBF amesema anachoona ni Klitschko kumuohopa kama David Haye.
  Lakini mjomba wa Fury na kocha wake, Peter Fury amepuuza madai hayo ya mpwa wake akisema; "Nimekuwa nikizungumza na kambi ya Klitschko na wamekuwa wazi sana kwetu. Nilimuambia Tyson mapema, Huyu si David Haye, Wladimir atapigana na wewe. Anajua kama hatafanya hivyo ataacha wazi mataji yake yote, kitu ambacho si anachotaka kwa heshima yake,"amesema na kuongeza. "Nahangaikia kupanga upya tarehe ya pambano, na itakapokuwa tayari nitakujulisha,".
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KLITSCHKO AJITOA PAMBANO NA TYSON AKIDAI KUUMIA MAZOEZINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top