• HABARI MPYA

  Jumatatu, Septemba 21, 2015

  SIMBA SC HAOO UNGUJA, HANS POPPE AWAAMBIA YANGA; “TUTAWALISHA SUPU YA MAWE KWA KACHUMBARI YA PILIPILI MANGA NA TOMATO”

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  WAKATI kikosi cha Simba SC kinaondoka leo kwenda Zanzibar kuweka kambi, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu hiyo, Zacharia Hans Poppe (pichani juu )amewaambia mahasimu, Yanga SC wasubiri supu ya mawe kwa kachumbari ya pilipili manga na tomato Jumamosi wiki hii.
  Mahasimu, Simba inayofundishwa na Muingereza Dylan Kerr na Yanga ya Mholanzi, Hans van der Pluijm ambayo tayari ipo kisiwani Pemba tangu jana, watamenyana wikiendi hii katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, timu zote zikitoka kushinda mechi tatu za awali.
  Yanga imezifunga Coastal Union 2-0, Prisons 3-0 na JKT Ruvu 4-1 juzi, wakati Simba SC imezifunga 1-0 African Sports, 2-0 Mgambo na jana 3-1 Kagera Sugar. 
  Na Hans Poppe amesema baada ya ushindi wa 3-1 jana sasa wanakwenda kambini Zanzibar kuiandalia Yanga SC ‘dozi nene’ na amewataka wapinzani wao hao wa jadi wakae tayari.
  “Yanga SC wanapiga sana kelele, imekuwa timu ya magazetini, inasifiwa sana wakati uwanjani haina lolote. Sasa wasubiri supu ya mawe iliyochanganywa na kachumbari, pilipili manga na tomato Jumamosi,”amesema. 
  Kikosi cha Simba SC kilichoifunga 3-1 Kagera Sugar jana
  Kikosi kizima cha Simba SC kinatarajiwa kuondoka Dar es Salaam leo kwenda Zanzibar kwa kambi ya wiki moja.
  Makipa; Vincent De Paul Angban, Peter Manyika
  Denis Deonis Richard.
  Mabeki; Mohamed Hussein, Hassan Ramadhani Kessy, Emery Nimubona, Samih Hajji Nuhu, Hassan Isihaka, Murushid Juuko, Mohamed Fakhi na Said Issa,
  Viungo; Abdi Banda, Jonas Mkude, Justice Majabvi, Awadh Juma, Saidi Hamisi Ndemla, Mwinyi Kazimoto, Peter Mwalyanzi, Simon Serunkuma na Joseph Kimwaga.
  Washambuliaji; Ibrahim Hajibu, Issa Abdallah, Daniel Lyanga, Boniphace Maganga, Hamisi Kizza, Pape Abdoulaye Ndaw na Nahodha Mussa Hasan Mgosi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA SC HAOO UNGUJA, HANS POPPE AWAAMBIA YANGA; “TUTAWALISHA SUPU YA MAWE KWA KACHUMBARI YA PILIPILI MANGA NA TOMATO” Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top