• HABARI MPYA

  Jumatano, Septemba 23, 2015

  TWIGA STARS KUJIPIMA NA MALAWI OKTOBA 24

  TIMU ya taifa ya Wanawake ya Tanzania, Twiga Stars inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Taifa ya Wanawake ya Malawi tarehe 24 Oktoba, mwaka huu nchini Malawi.
  Mechi hiyo kati ya Twiga Stars dhidi ya Malawi itachezwa jijini Lilongwe kufuatia mwaliko wa chama cha soka nchini Malawi (FAM) kuialika Twiga Stars kwenda nchini Malawi kwa ajili ya mchezo huo
  Mchezo huo wa kirafiki ni sehemu ya maandalizi ya vikosi vya timu zote mbili za Wanawake Tanzania na Malawi kwa ajili ya michuano mbalimbali.Mwenyekiti wa Chama cha Soka ya Wanawake Tanzania (TWFA), Amina Karuma anatarajiwa kuhudhuria kuhudhuria kongamano la viongozi wa soka la wanawake duniania litakalofanyika Zurich nchini Uswisi Septemba 28 – 02 Oktoba, 2015.
  Kongamano hilo linashirkisha viongozi 35 wanawake wa mpira wa miguu kutoka semehu mbalimbali duniani ikiwa ni muendelezo wa kongamano liliofanyika mwezi Machi mwaka huu Vancouver Canada wakati wa fainali za kombe la Dunia la Wanawake.
  Programu hiyo ya viongozi wa wanawake ni sehemu ya mikakati ya FIFA ya kuongeza idadi ya viongozi wengi wa soka wanawake duniani katika utawala wa mpira wa miguu wa wanawake.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TWIGA STARS KUJIPIMA NA MALAWI OKTOBA 24 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top