• HABARI MPYA

  Jumapili, Septemba 20, 2015

  JOHN BOCCO AING’ARISHA AZAM FC MWADUI, AGGREY MORRIS ALIMWA ‘MWEKUNDU’, SAID BAHANUZI ATAKATA MANUNGU

  MATOKEO MECHI ZA LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA
  Jumapili Sept 20, 2015
  Mwadui FC 0-1 Azam FC 
  Mtibwa Sugar 2-1 Ndanda FC
  Simba SC 3-1 Kagera Sugar
  Coastal Union 0-0 Toto Africans
  Jana Septemba 19, 2015
  Stand United 2-0 African Sports
  Mgambo Shooting 1-0 Majimaji FC
  Prisons 1-0 Mbeya City
  Yanga SC 4-1 JKT Ruvu
  Nahodha John Bocco ameifungia bao pekee Azam Fc ikishinda 1-0 Mwadui

  BAO pekee la Nahodha John Raphael Bocco limeipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji Mwadui FC Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Huo unakuwa ushindi wa tatu mfululizo kwa Azam FC inayofundishwa na Muingereza Stewart Hall, baada ya awali kushinda 2-1 dhidi ya Prisons Uwanja wa azam Comolex, Chamazi, Dar es Salaam na 2-0 dhidi ya Stand United Uwanja Kambarage, Shinyanga.
  Azam FC sasa inashuka hadi nafasi ya tatu nyuma ya Simba SC, zikiwa na pointi sawa na Yanga SC, tisa kila moja, lakini zinazidiana kwa wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa. 
  Katika mchezo wa leo, Azam FC ilipata pigo baada ya Nahodha wake, Aggrey Morris kutolewa kwa kadi nyekundu, wakati mshambuliaji wa Mwadui FC, Rashid Mandawa alikosa penalti. 
  Mechi nyingine za leo, Mtibwa Sugar imeshinda 2-1 dhidi ya Ndanda FC Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro mabao yake yakifungwa na Salum Mbonde na Said Bahanuzi la wageni likifungwa na Kiggi Makassy, wakati Coastal Union imelazimishwa sare ya 0-0 na Toto Africans Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: JOHN BOCCO AING’ARISHA AZAM FC MWADUI, AGGREY MORRIS ALIMWA ‘MWEKUNDU’, SAID BAHANUZI ATAKATA MANUNGU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top