• HABARI MPYA

  Jumatatu, Septemba 21, 2015

  PENALTI YA MESSI 'YAOTA MBAWA' BARCELONA YASHINDA 4-1 NA KUREJEA KILELENI LA LIGA

  TIMU ya Barcelona imeshinda mabao 4-1 dhidi ya Levante katika mchezo wa Jumapili, lakini Mwanasoka Bora wa Ulaya, Lionel Messi amekosa penalti Uwanja wa Camp Nou.
  Messi alimpa pasi nzuri Marc Bartra kuifungia Barca bao la kwanza dakika ya 50, kabla ya yeye mwenyewe kufunga la tatu kwa penalti dakika ya 61 kufuatia Neymar kufunga la pili dakika ya 56.
  Levante walipata bao la kufutia machozi kupitia kwa Victor dakika ya 66 kabla ya Messi kukosa penalti baada ya kupaisha, lakini akarekebisha makosa kwa kufunga bao la nne dakika ya 90. 
  Barcelona sasa inarejea kileleni mwa La Liga kwa rekodi ya asilimia 100 baada ya kushinda mechi zao zote nne msimu huu. 
  Lionel Messi (kushoto) na Neymar wakishangilia ushindi wa 4-1 dhidi ya Levante leo PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: PENALTI YA MESSI 'YAOTA MBAWA' BARCELONA YASHINDA 4-1 NA KUREJEA KILELENI LA LIGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top