• HABARI MPYA

  Jumapili, Septemba 27, 2015

  SIMBA SC WAMSHUSHIA SHUTUMA NZITO NKONGO, WADAI ETI ALIFIKIA HADI KUWATUKANA WACHEZAJI WAO

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  SIMBA SC imesema katika mchezo wa jana haikutendewa haki na refa Israel Mujuni, ambaye alifikia hadi kuwatukana wachezaji wao.
  Ofisa Habari wa Simba SC, amesema kwamba Nkongo kwa dhamira ya kusudi jana aliamua kuwatoa mchezoni wachezaji wao kwa kuwapa kadi kwa rafu sawa na amabazo walicheza wachezaji wa Yanga bila kuadhibiwa.
  "Tumshukuru Mungu kwa kutuwezesha kumaliza mchezo huo salama, Mungu ashukuriwe sana pamoja na wapenzi wetu pia. Sababu mashabiki wetu wameonyesha utulivu wa kiunamichezo kwa kutokufanya fujo yoyote licha ya mwamuzi wa mchezo huo, Israel Nkongo kuharibu mchezo kwa makusudi,"amesema.
  Refa Israel Nkongo (mwenye mpira) akiziongoza timu kuingia uwanjani jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

  Amesema kilichoshangaza mashabiki wote waliokuwa uwanjani na walioangalia kwenye Televisheni ni kumuacha mchezaji wa Yanga, Donald Ngoma kuendelea na mchezo licha ya kumpiga kichwa cha makusudi beki wa Simba, Hassan Kessy.
  "Mbali ya vitendo hvyo wachezaji wetu wametulalamikia kutukanwa na mwamuzi wa mchezo huo Nkongo,"ameongeza Manara, mtoto wa kiungo wa zamani wa Yanga SC, Sunday Manara 'Kompyuta'.
  Manara amesema Simba SC wanaamini TFF watachunguza malalamiko yao na kuchukua hatua stahiki kwa mwamuzi huyo, ambaye kila mtu aliyeuona mchezo huo anakiri kuwa alishindwa kuumudu.
  "Sisi Simba tumeyakubali matokeo hayo ya dakika tisini za mchezo na tutumie nafasi hii kiungwana kabisa kuwapongeza watani wetu wa jadi kwa ushindi huo walioupata,".
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA SC WAMSHUSHIA SHUTUMA NZITO NKONGO, WADAI ETI ALIFIKIA HADI KUWATUKANA WACHEZAJI WAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top