• HABARI MPYA

  Jumamosi, Septemba 26, 2015

  ULIMWENGU AIFUNGIA BAO MUHIMU MAZEMBE IKICHAPWA 2-1 NA MERREIKH

  Thomas Ulimwengu ameifungia bao muhimu TP Mazembe leo
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu amefunga bao pekee la TP Mazembe ikichapwa mabao 2-1 na wenyeji El Merreikh ya Sudan.
  Katika mchezo huo wa Nusu Fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Ulimwengu alifunga bao hilo dakika ya 77 akimalizia pasi ya Rogger Assale, ambalo lilikuwa la kusawazisha baada ya mshambuliaji Mghana, Francis Coffie kutangulia kuwafungia wenyeJi dakika ya 41.  
  Na alifunga bao hilo dakika mbili tu baada ya kutokea benchi kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Rainford Kalaba dakika ya 75.
  Hata hivyo, Bakri Al Madina aliifungia Merreikh bao la ushindi dakika ya 80, akimalizia pasi ya Ragei Abdalla.
  Sasa Mazembe watatakiwa kushinda 1-0 wiki ijayo mjini Lubumbashi DRC ili kutinga fainali.
  Kikosi cha Mereikh kilikuwa; J. Salim, Ala'a Eldin Yousif, Musaab Omer, Ayman Saied/ Omar Bakheet dk73, Ragei Abdalla, Amir Kamal, Ramadan Agab, D. Libere, Bakri Al Madina, S. Jabason na Francis Coffie.
  TP Mazembe; R. Kidiaba , J. Kasusula/M. Bokad dk58, Y. Frimpong, J. Kimwaki, S. Coulibaly, B. Diarra, D. Adjei Nii/ N. Sinkala dk58, R. Kalaba/ T. Ulimwengu dk75, M. Samatta, R. Assale na A. Traore.
  Katika Nusu Fainali ya Kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika, wenyeji Orlando Pirates ya Afrika Kusini wameshinda 1-0 dhidi ya Al Ahly ya Misri.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ULIMWENGU AIFUNGIA BAO MUHIMU MAZEMBE IKICHAPWA 2-1 NA MERREIKH Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top