• HABARI MPYA

  Jumapili, Septemba 27, 2015

  MOTO UNAWAKA CHAMAZI LEO AZAM FC NA MBEYA CITY

  RATIBA NATOKEO YA LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA
  Leo; Septemba 27, 2015
  Azam Fc Vs Mbeya City
  African Sports Vs Ndanda FC
  Jana; Septemba 26, 2015
  Simba SC 0-2 Yanga SC
  Coastal Union 0-0 Mwadui FC
  Prisons FC 1-0 Mgambo JKT
  JKT Ruvu 0-1 Stand United
  Mtibwa Sugar 1-0 Majimaji FC
  Kagera Sugar 0-0 Toto Africans

  LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, inatarajiwa kuendelea leo kwa mechi mbili Tanga na Dar es Salaam.
  Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam, wenyeji Azam FC watawakaribisha Mbeya City, wakati Uwanja wa Mkwakwani, Tanga wenyeji African Sports watawakaribisha Ndanda FC ya Mtwara.
  Macho na masikio ya wengi yanatarajiwa kuelekezwa Uwanja wa Azam, ambako timu mbili zenye upinzani zitakuwa zikimenyana.
  Azam FC inahitaji ushindi leo ili kuzifikia Yanga SC na Mtibwa Sugar kwa pointi kileleni, wakati Mbeya City pia inahitaji ushindi ili kujiweka katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa Ligi Kuu.
  Yanga SC inaongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 12 sawa na Mtibwa Sugar iliyo katika nafasi ya pili, wakati Simba SC ya tatu kwa pointi zake tisa sawa na Azam FC.
  Azam FC leo itamkosa beki wake ‘kisiki’ Aggrey Morris aliyeonyeshwa kadi nyekundu katika mchezo uliopita dhidi ya Mwadui FC Shinyanga, lakini kocha Muingereza Stewart Hall hataumiza kichwa sana, kwani ana mabeki wengine watatu wa kati, Said Mourad, David Mwantika na Racine Diouf.
  Kipa maarufu, Juma Kaseja anatarajiwa kuonekana tena mbele ya mashabiki Dar es Salaam akiidakia Mbeya City baada ya msimu mmoja wa kuwa nje kufuatia kujiondoa Yanga SC.     
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MOTO UNAWAKA CHAMAZI LEO AZAM FC NA MBEYA CITY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top