• HABARI MPYA

  Alhamisi, Septemba 24, 2015

  LIVERPOOL YAPITA KWA MBINDE KOMBE LA LIGI, MAN UNITED, ARSENAL NA CHELSEA NAZO ZAPETA

  MATOKEO MECHI ZA KOMBE LA LIGI JUZI NA JANA

  Septemba 23, 2015
  Manchester United 3 - 0 Ipswich Town
  Liverpool (3) 1 - 1 (2) Carlisle United
  Newcastle United 0 - 1 Sheffield Wednesday
  Norwich City 3 - 0 West Bromwich Albion
  Crystal Palace 4 - 1 Charlton Athletic
  Tottenham Hotspur 1 - 2 Arsenal
  Walsall 1 - 4 Chelsea
  MK Dons 0 - 6 Southampton
  Septemba 22, 2015  
  Reading 1 - 2 Everton
  Hull City 1 - 0 Swansea City
  Sunderland 1 - 4 Manchester City
  Aston Villa 1 - 0 Birmingham City
  Leicester City 2 - 1 West Ham United
  Preston North End (2) 2 - 2 (3) Bournemouth
  Middlesbrough 3 - 0 Wolverhampton 

  Kipa wa Liverpool, Adam Bogdan akiokoa penalti moja kati ya tatu jana katika mchezo wa Kombe la Ligi, maarufu kama Capital One Cup jana PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  KIPA mpya wa Liverpool, Adam Bogdan usiku wa jana alikuwa shujaa Uwanja wa Anfield baada ya kuokoa penalti tatu na kuiwezesha timu hiyo kutinga Raundi ya Kombe la Ligi England.  
  Liverpool ilishinda kwa penalti 3-2 baada ya sare ya 1-1 na Carlisle ya Ligi Daraja la Nne England katika michuano ya Capital One.
  Mchezaji mwingine mpya, Danny Ings alianza kuifungia Liverpool kipindi cha kwanza kabla ya  Derek Asamoah kuisawazishia Carlisle na mchezo ukaenda kwenye dakika 30 za nyongeza.
  Penalti za Liverpool zilifungwa na Milner, Can na Ings wakati Lallana na Coutinho walikosa na za Carlisle zilifungwa na Dicker na Mcqueen huku Grainger, Joyce na Hery wakikosa.
  Kikosi cha Liverpool kilikuwa: Bogdan, Clyne/Ibe dk86, Lovren, Milner, Firmino/Origi dk35, Moreno, Lallana, Can, Allen/Coutinho dk64, Ings na Skrtel.
  Carlisle: Gillespie, Miller, Raynes, Grainger, McQueen, Kennedy/Gillesphey dk73, Dicker, Joyce, Sweeney/Ibehre dk65, Hery na Asamoah/Gilliead dk64. Wayne Rooney looks to the sky and celebrates as he opens the scoring against Ipswich at Old Trafford
  Nahodha wa Man United, Wayne Rooney akiangalia mawinguni kushangilia baada ya kufunga jana dhidi ya Ipswich Uwanja wa Old Trafford PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  MECHI NYINGINE ZA JUZI NA JANA...
  Manchester United imeshinda 3-0 dhidi ya Ipswich Town, mabao ya Wayne Rooney dakika ya 23, Andreas Pereira dakika ya 60 na Anthony Martial dakika ya 90+2 Uwanja wa Old Trafford, Newcastle United imefungwa 1-0 nyumbani na  Sheffield Wednesday bao pekee la Lewis McGugan Uwanja wa St. James' Park.
  Arsenal imeshinda 2-1 ugenini dhidi ya Tottenham Hotspur Uwanja wa White Hart Lane, mabao yake yakifungwa na Mathieu Flamini dakika ya 26 na 78, huku pia Calum Chambers akijifunga dakika ya 56 kuipa Spurs bao moja.
  Chelsea pia imeshinda 4-1 ugenini, mabao yake yakifungwa na Ramires Santos do Nascimento dakika ya 10, Loic Remy dakika ya 41, Robert Kenedy Nunes do Nascimento dakika ya 52 na Pedro Rodriguez Ledesma dakika ya 90+2 Uwanja wa Bescot, huku bao pekee la wenyeji likifungwa na James O'Connor dakika ya 46).
  Southampton imeifumua 6-0 MK Dons, mabao yake yakifungwa na Jay Rodriguez dakika ya tano na 48 kwa penalti, Sadio Mane dakika ya 10 na 25 na Shane Long dakika ya 68 na 75, wakati Everton pia imeshinda 2-1 ugenini dhidi ya Reading mabao yake yakifungwa na Ross Barkley dakika ya 62 na Gerard Deulofeu dakika ya 73, huku bao la wenyeji likifungwa na  Nick Blackman dakika ya 36 Uwanja wa Madejski.Ramires wheels away and does a somersault in celebration after claiming his first goal for the Blues since April
  Ramires akibinuka sarakasi kushangilia baada ya kuifungia The Blues kwa mara ya kwanza tangu Aprili PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Norwich City imeshinda 3-0 dhidi ya West Bromwich Albion, mabao ya Matthew Jarvis dakika ya 62, Kyle Lafferty dakika ya 85 na Sebastien Pocognoli aliyejifunga dakika ya 90 Uwanja wa Carrow Road, Crystal Palace imeshinda 4-1 dhidi ya Charlton Athletic mabao yake yakifungwa na Fraizer Campbell dakika ya 51, Dwight Gayle matatu, mawili kwa penalti dakika ya 59 na 74 na lingine dakika ya 86, huku Mahamadou-Naby Sarr akifunga bao pekee la wapinzani dakika ya 65 Uwanja wa Selhurst Park.
  Juzi Stoke City iliifunga 1-0 Fulham bao pekee la Peter Crouch dakika ya 33 Uwanja wa Craven Cottage, Hull City iliifunga 1-0 Swansea City bao pekee la David Meyler dakika ya 41 Uwanja wa KC.
  Manchester City iliichapa 4-1 Sunderland mabao yake yakifungwa na Sergio Aguero kwa penalti dakika ya tisa, Kevin De Bruyne dakika ya 25, Vito Mannone (aliyejifunhga dakika ya 33 na Raheem Sterling dakika ya 36 Uwanja wa Light wakati Aston Villa iliifunga 1-0 Birmingham City bao pekee la Rudy Gestede dakika ya 62 Uwanja wa  
  Villa Park.
  Leicester City imeshinda 2-1 dhidi ya West Ham United, Bournemouth imeitoa Preston North End kwa penalti 3-2 baada ye sare 2-2, Middlesbrough imeifunga 3-0 Wolverhampton Wanderers mabao ya Albert Adomah dakika ya 37 na 64 na Diego Fabbrini dakika ya 57 Uwanja wa Riverside. Flamini points to the sky in celebration after giving the Gunners the lead against fierce London rivals Tottenham on 26 minutes
  Flamini akinyoonsha kidole angani kushangilia baada ya The Gunners  PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  RATIBA KAMILI RAUNDI YA NNE KOMBE LA LIGI ENGLAND
  Manchester City v Crystal Palace
  Liverpool v Bournemouth
  Manchester United v Middlesbrough
  Everton v Norwich
  Southampton v Aston Villa
  Sheffield Wednesday v Arsenal
  Hull v Leicester
  Stoke v Chelsea
  (Mechi zitachezwa Oktoba 26, mwaka huu) 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YAPITA KWA MBINDE KOMBE LA LIGI, MAN UNITED, ARSENAL NA CHELSEA NAZO ZAPETA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top