• HABARI MPYA

  Ijumaa, Septemba 25, 2015

  CHUCHU HANS: WASANII KUPIGIA DEBE WANASIASA MBONA POA TU

  Chuchu kulia akiwa na Vincent Kigosi 'Ray'
  KUFUATIA madai ya wasanii wengine wengi wanaosema kuwa, msanii kujiingiza kwenye siasa ni kuishiwa, nyota wa kike wa filamu za Kibongo Chuchu Hans ameibuka na kujitetea. 
  Akizungumza na SALUTI5 Chuchu amesema, sanaa na siasa vina uhusiano mkubwa na kwamba mtu anapojitumbukiza kwenye sanaa tu anakuwa tayari ni mwanasiasa hata kama hajatangaza nia.   
  “Mi nafikiri ni mawazo duni tu ya baadhi ya wenzetu kudai kuwa, msanii kuingia kwenye siasa ni kuishiwa,” alisema Chuchu Hans huku akibainisha kuwa binafsi, yeye ni mwanasiasa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CHUCHU HANS: WASANII KUPIGIA DEBE WANASIASA MBONA POA TU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top