• HABARI MPYA

  Jumapili, Septemba 20, 2015

  YANGA SC WAINGIA KAMBINI PEMBA LEO KUJIANDAA NA ‘MNYAMA’ SEPTEMBA 26

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  YANGA SC imeingia kambini Pemba leo kujiandaa na mchezo dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Simba SC wiki ijayo.
  Ni mchezaji mmoja tu, kipa wa nne Benedicto Tinocco ambaye hakupanda ndege kwenda kisiwani kwa maandalizi ya mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm wa Yanga SC amechagua Pemba kwa sababu ya utulivu na mandhari kuelekea mchezo huo wa Septemba 26 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
  Kikosi cha Yanga SC kilichofiunga JKT Ruvu 4-1 jana

  Kikosi cha Yanga SC kilichoigia kambini Pemba ni makipa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Mudathir Khamis na Deogratius Munishi ‘Dida’.
  Mabeki; Juma Abdul, Oscar Joshua, Mwinyi Haji Mngwali, Pato Ngonyani, Kevin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Mbuyu Twite, Vincent na Bossou.
  Viungo; Salum Telela, Andrey Coutinho, Haruna Niyonzima, Thabani Kamusoko, Said Juma, Godfrey Mwashiuya, Deus Kaseke na Simon Msuva.
  Washambuliaji; Mateo Anthony Simon, Donald Ngoma, Malimi Busungu na Amisi Tambwe.
  Mahasimu, Simba inayofundishwa na Muingereza Dylan Kerr na Yanga watamenyana wikiendi ijayo katika mfululizo wa Ligi Kuu, timu zote zikitoka kushinda mechi tatu za awali.
  Yanga imezifunga Coastal Union 2-0, Prisons 3-0 na JKT Ruvu 4-1 jana, wakati Simba SC imezifunga 1-0 African Sports, 2-0 Mgambo na leo 3-1 Kagera Sugar. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA SC WAINGIA KAMBINI PEMBA LEO KUJIANDAA NA ‘MNYAMA’ SEPTEMBA 26 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top