• HABARI MPYA

  Jumapili, Septemba 20, 2015

  DANNY MRWANDA AENDA KUIPANDISHA LIPULI

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  ALIYEKUWA mshambuliaji wa Yanga SC, Danny Davis Mrwanda amesajiliwa na Lipuli ya Iringa inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara.
  Mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba SC, alitemwa Yanga SC baada ya nusu msimu kutokana na sababu za kibinafsi zaidi na sasa ameamua kwenda kujaribu kuirejesha Ligi Kuu Lipuli.
  Danny Mrwanda (kulia) akifurahia na Simon Msuva baada ya kufunga bao wakati anacheza Yanga SC msimu uliopita

  Kikosi kamili cha Lipuli ni; Adam Omary Soba, Green Paul Jerosi, Hamisi Shabani Likwena, Shirazy Abdallah Sozigwa, Kessy Christian Ntale, Markyard Franco, Abdul Salum Kussi, Mwamba Timothy Mkumbwa, Lulanga Andrew Mapunda na 
  Ramadhani Hussein Ramadhani. 
  Wengine ni Meshack Abel Mwankina, Mohamed Said Mpopo, Abdi Yassin Mtangi, Deograsias Anthony Kulwa, Zamogoni Michael Pangapanga, Majid Musa Said, Haji Juma Mapunda na Mathayo Hezron Wilson.
  Wamo pia Marko Kuga, Stone Peter Mwanyilu, Dany Davis Mrwanda, Fadhili Said Butamu, Dismas Yustus Achimpate, Yona Ndibila, Sultan Mwenegoha Kassim, Hamisi Kisengo, Kashiru Salum na Geofrey Kombole.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: DANNY MRWANDA AENDA KUIPANDISHA LIPULI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top