• HABARI MPYA

  Jumapili, Septemba 27, 2015

  YANGA B WALIANZA KUWATILIA 'BARAKA' KAKA ZAO, WALIICHAPA SIMBA B 3-2

  Wachezaji wa Yanga B wakishangilia baada ya kupata bao la tatu katika ushindi wa 3-2 dhidi ya Simba SC mchana wa Jumamosi Uwanja Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa utangulizi, kabla ya mechi ya kaka zao ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ambayo Yanga SC ilishinda pia 2-0 kwa mabao ya Amissi Tambwe na Malimi Busungu. Mabao ya Yanga B yalifungwa na Said Mussa kwa penalti dakika ya tano, Benito Michael dakika ya 59 na Ayoub M. Ayoub dakika ya 90, wakati ya Simba B yalifungwa na Raji Mohammed dakika ya 59 na Hussein Hamisi dakika ya 88.
  Beki wa Yanga SC, Hamisi Hajji (kulia) akitafuta maarifa ya kumpita mshambuliaji wa Simba SC, Moses Kibindu
  Benito Michael wa Yanga B (kushoto) akipambana na Mohammed Mussa wa Simba B (kulia)

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA B WALIANZA KUWATILIA 'BARAKA' KAKA ZAO, WALIICHAPA SIMBA B 3-2 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top