• HABARI MPYA

    Wednesday, September 30, 2015

    YANGA SC HAWAKAMATIKI, MTIBWA SUGAR YATANDIKWA 2-0 JAMHURI…NGOMA NA BUSUNGU WAZIMA NGEBE ZA WAKATA MIWA

    MECHI ZIJAZO LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA
    Septemba 30, 2015
    African Sports 0-1 Mgambo 
    Azam FC 2-0 Coastal Union
    Kagera Sugar 0-0 JKT Ruvu
    Mtibwa Sugar 0-2 Yanga SC
    Majimaji FC 1-1 Ndanda FC
    Prisons 0-0 Mwadui FC
    Simba SC 1-0 Stand United
    Kesho; Oktoba 1, 2015
    Toto Africans Vs Mbeya City
    Kikosi cha Yanga SC kilichoifunga Mtibwa Sugar 2-0 leo Uwanja wa Jamhuri

    Na Prince Akbar, MOROGORO
    YANGA SC imeendelea kung’ang’ania usukani wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kufuatia ushindi wa mabao 2-0 jioni ya leo dhidi ya wenyeji Mtibwa Sugar, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
    Shukrani kwao, wafungaji wa mabao hayo Malimi Busungu dakika ya 53 na Mzimbabwe Donald Ngoma dakika ya 89 katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Erick Onoka wa Arusha.
    Yanga SC sasa inafikisha pointi 15 sawa na Azam FC baada ya timu zote kucheza mechi tano, lakini wana Jangwani wanakaa kileleni kwa wastani wao mzuri wa mabao.
    Mechi nyingine za Ligi Kuu jioni ya leo, Mgambo JKT imeifunga 1-0 African Sports Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, Azam FC imeichapa 2-0 Coastal Union Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam na Kagera Sugar imetoka sare ya 0-0 na JKT Ruvu Uwanja wa A.H. Mwinyi, Tabora.
    Mechi nyingine, Majimaji FC imetoka sare ya 1-1 na Ndanda FC Uwanja wa Majimaji, Songea, Prisons imetoka 0-0 na Mwadui FC Uwanja wa Sokoine, Mbeya na Simba SC imeshinda 1-0 dhidi ya Stand United Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
    Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inayoonyeshwa moja kwa moja na Azam TV, itaendelea kesho kwa mchezo mmoja tu, kati ya wenyeji Toto Africans na Mbeya City kesho Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
    Kikosi cha Mtibwa Sugar kilikuwa; Said Mohamed, Rodgers Freddy, Issa Rashid, Andrew Vicent, Salim Mbonde, Shabani Nditi, Vicent Barnabas, Mzamiru Yassin, Seleman Rajab, Mohamed Ibrahim/Said Bahanuzi dk68 na Shiza Kichuya/Jaffar Salum dk60.
    Yanga SC; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, Mwinyi Hajji Mngwali, Nadir Haroub 'Cannavaro', Kelvn Yondan, Said Juma 'Makapu', Malimi Busungu, Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe/Mateo Anthony Simon dk85, Donald Ngoma na Salum Telela.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC HAWAKAMATIKI, MTIBWA SUGAR YATANDIKWA 2-0 JAMHURI…NGOMA NA BUSUNGU WAZIMA NGEBE ZA WAKATA MIWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top