• HABARI MPYA

  Jumapili, Septemba 20, 2015

  MANYIKA NDIYE ‘SIMBA ONE’ MPYA, KIPA WA CHELSEA AENDELEA ‘KUYACHOMA’ MSIMBAZI

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  NAAM, sasa unaweza kumuita ndiye Simba One, baada ya kuondoka kwa Ivo Mapunda.
  Kipa ‘dogo’ Peter Manyika anaanza kwa mara ya tatu mfululizo katika kikosi cha Simba SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya kagera Sugar Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Kipa Vincent Angban raia wa Ivory Coast aliyewahi kudakia U21 ya Chelsea ya England, ambaye amesajiliwa Simba SC msimu huu- ameendelea kusubiri mbele ya Manyika ambaye msimu uliopita alikuwa anasubiri kwa Ivo mapunda.
  Manyika anaanza kwa mara ya tatu mfululizo leo Simba SC

  Manyika aliyedaka kwa ustadi mkubwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga Simba SC ikivuna pointi sita katika mechi zake mbili za awali za Ligi Kuu, leo ameanzishwa tena Dar es Salaam.
  Manyika hakuruhusu bao Simba SC ikishinda 1-0 na African Sports na 2-0 na JKT Mgambo, tena akiokoa michomo kadhaa ya hatari.
  Kocha Muingereza, Dylan Kerr amewapumzisha mabeki Hassan Ramadhani Kessy na Mganda Juuko Murushid, badala yao wakianza Emery Nimubona beki ya kulia na kiungo Mzimbabwe Justuce Majabvi atacheza katikati pamoja na Hassan Isihaka.
  Kikosi kinachoanza Simba SC ni; Peter Manyika, Emery Nimubona, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Hassan Isihaka, Justuce Majabvi, Awadh Juma, Simon Sserunkuma, Said Ndemla, Ibrahim Hajib, Hamisi Kiiza na Peter Mwalyanzi
  Kwenye benchi watakuwepo Angabn, Kessy, Said Issa, Mwinyi Kazimoto, Pape Abdoulaye N’daw, Boniface Maganga na Joseph Kimwaga.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MANYIKA NDIYE ‘SIMBA ONE’ MPYA, KIPA WA CHELSEA AENDELEA ‘KUYACHOMA’ MSIMBAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top