• HABARI MPYA

    Wednesday, April 15, 2015

    PACQUIAO KUGOMBEA URAIS WA UFILIPINO AKISTAAFU NDONDI

    BONDIA Manny Pacquiao amepanga kugombea Urais wa nchini mwake, Ufilipino atakapoacha ngjumi.
    Kwa matokeo yoyote yale katika pambano lake na Floyd Mayweather Jr. Mei 2, mwaka huu, bado Pacquiao atakuwa na ndoto za kuwa mtu wa kutawala kwenye vyombo vya habari.
    Kwa mujibu wa promota Bob Arum, wakati Pacquiao atakapoamua kutungika glavu zake moja kwa moja atajitosa kikamilifu kwenye siasa kwa kupoanda ngazi za juu zaidi kutoka ya ubunge anayoshikilia sasa.
    "Atakuwa Rais," amesema Arum. Akiwa na umri wa miaka 32, Pacquiao alichaguliwa katika Bunge la Ufilipino na kwa mujibu wa Arum, bondia huyo atahamia katika nafasi ya useneta mwaka 2016. Kisha mwamka 2022 au baadaye,  atawania Urais wa Ufilipino.
    "Nafikiri mustakabali wa kisiasa," Arum amesema.Kumbuka Pacquiao amerekodi wimbo wa kupandia ulingioni kwenye paambano hilo la Karne uitwao "Lalaban Ako Para Sa Filipino" au "I Will Fight for the Filipino," yaani nitapigana kwa ajili ya Ufilipino. Kumpiga Mayweather Jr. itakuwa dalili ya kwanza ya ushindi katika kampeni zake za kugombea Urais.
    Manny Pacquiao has big plans after his boxing career ends.  (Getty Images)
    Manny Pacquiao ana mipango mikubwa atakaopostaafu ndondi
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PACQUIAO KUGOMBEA URAIS WA UFILIPINO AKISTAAFU NDONDI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top